Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 18; Hakuna Anayejali Maisha Yako Zaidi Yako Mwenyewe.

By | January 18, 2015

Kuna wakati ambapo tunajali sana kuhusu watu wengine wanavyojali kuhusu maisha yetu. Tunafikiri kwamba watu wengine wanatufuatailia kila tunachofanya na hivyo kuhofia watatuchukuliaje hasa kama tutashindwa. SOMA; Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku. Ukweli ni kwamba hakuna anayejali maisha yako zaidi yako mwenyewe. Hakuna ambaye anakosa usingizi (more…)

UKURASA WA 17; Hofu, Matumizi Mabaya Ya Ubunifu Wako.

By | January 17, 2015

Hofu, hiki ni kikwazo cha watu wengi sana kufikia malengo yao na hata mafanikio makubwa. Hofu ni matumizi mabaya ya ubunifu mkubwa ulioko ndani yako. Kila mtu anaubunifu na anaweza kutumia mawazo yake kutengeneza picha kubwa sana ya kuboresha maisha yake na ya wale ambao wanawazunguka. Kwa kutumia uwezo huu (more…)

UKURASA WA 16; Jijengee Utaratibu Wa Kila Siku.

By | January 16, 2015

Sehemu kubwa ya mambo unayofanya kila siku unafanya kutokana na tabia ambayo tayari umeshajijengea. Kwa mfano unapoamka asubuhi huenda huwa unasafisha kinywa chako, hii ni tabia uliyoijenga kwa muda mrefu sana na hivyo hutumii nguvu yoyote kuifanya. Yaani huanzi kufikiria kama usafishe kinywa au la, ukiamka tu mpja kwa moja (more…)

UKURASA WA 15; Afya Yako Ni Kitu Muhimu Sana.

By | January 15, 2015

Katika vitu muhimu sana kwenye maisha yako, cha kwanza ni afya yako. Haijalishi una malengo na mipango mizuri kiasi gani kama afya yako ni mbovu hutaweza kufika popote. Na kama kwenye kipigania malengo yako, umeisahau afya yako, unaweza kushindwa kufurahia kile unachokipata hasa unapokuwa na afya mbovu. Kwa mfano utakuwa (more…)

UKURASA WA 14; Kataa Kupokea Chochote Kizuri, Na Kubali Hiki…

By | January 14, 2015

Unapoamua kuboresha maisha yako, hakikisha kila kitu kinakuwa bora. Jambo moja la kushangaza kuhusu maisha ni kwamba unapokataa kupokea ambacho sio bora, lazima unapata kilicho bora. Unapokataa kupokea kile unachokiona kizuri sasa, utapigana kupata kile kilichobora zaidi. Kataa kufanya kazi ambayo sio bora na hatimaye utaongeza juhudi ili kuifanya iwe (more…)

UKURASA WA 13; Jifunze Kila siku.

By | January 13, 2015

Hitaji la chini kabisa la wewe kufikia mafanikio kwenye eneo lolote kwenye maisha yako ni kujifunza kila siku. Ni muhimu sana wewe kujifunza kila siku, jifunze kuhusiana na kazi au biashara unayofanya, jifunze kuhusiana na maendeleo binafsi, jifunze kuhusu fedha na uwekezaji na jifunze kuhusu maisha kwa ujumla. Dunia ya (more…)

UKURASA WA 12; Furaha Inatoka Ndani Yako Na Sio Kwa Watu Au Vitu.

By | January 12, 2015

Watu wengi wanafikiri kwamba kama wakiwa na watu wanaowapenda basi watakuwa na furaha kwenye maisha yao. Watu wengi wanafikiri kwamba wakiwa na fedha nyingi ndio watakuwa na furaha. Watu wengi wanafikiri kwamba wakishaondokana na changamoto za maisha ndio watakuwa na furaha. Watu wengi wanafikiri kwamba kama maisha yasingekuwa magumu wangekuwa (more…)

UKURASA WA 11; Watu Hawa Wanakurudisha Nyuma.

By | January 11, 2015

Hatimaye tupo ukurasa wa kumi na moja, kitabu chetu bado sana ila mabadiliko inabidi yaanze kuonekana mara moja. Mpaka sasa umeshakubali kwamba maisha yako yako chini yako, umeshaweka malengo makubwa ambayo unayapigania, umeshakubali kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na unabadili imani zako ili uweze kuwa na imani ya kuona (more…)

UKURASA WA 10; Umetengeneza Ulimwengu Wako Mwenyewe.

By | January 10, 2015

Upo hapo ulipo leo sio kwa sababu ya bahati au ajali, bali kwa sababu ndicho kitu ulichoamua kutengeneza mwenyewe. Maisha unayoishi leo ndio maisha uliyoamua kutengeneza mwenyewe, hujatengenezewa na wazazi wako, wala ndugu zako wala serikali yako. Ni wewe mwenyewe. Kila unachokifikiria kwa muda mrefu kwenye maisha yako ndio kinachotokea. (more…)

UKURASA WA 09; MUDA–Kitu Chenye Thamani Kubwa Ila Kisichothaminika Na Wengi.

By | January 9, 2015

Muda ni kitu chenye thamani kubwa sana kwenye maisha yako. Poteza fedha hata iwe nyingi kiasi gani, unaweza kuitafuta tena. Ila ukishapoteza muda ndio imetoka, huwezi kuutengeneza tena hata kama ungekuwa na fedha kiasi gani. Kitu kingine muhimu ni kwamba muda ndio kitu ambacho binadamu wote tumepewa kwa usawa. Watu (more…)