Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 08; Nidhamu Ndio Nguzo, Ukiikosa Utaanguka.

By | January 8, 2015

Moja ya vitu muhimu unavyotakiwa kuwa navyo ili uweze kufikia mafanikio ni nidhamu. Kwa kuwa na nidhamu(hasa nidhamu binafsi) utaweza kuweka malengo na mipango yako mwenyewe na kisha kuweza kuitekeleza. Ukikosa nidhamu utajikuta unashindwa kutekeleza kile ulichopanga mwenyewe na mwishowe ukashindwa kufanikiwa. Mwaka huu 2015 amua kujijengea nidhamu binafsi, amua (more…)

UKURASA WA 07; Uvumilivu Ni Nguzo Muhimu.

By | January 7, 2015

Japo umeshaamua kuchukua hatamu ya maisha yako na kukubali wewe pekee ndio unayeweza kubadili maisha yako… Japo umeshaweka malengo na mipango ambayo unaifanyia kazi ili mwaka huu uwe wa tofauti kwako… Japo umeshachagua kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kujua kwamba kazi ni muhimu sana… Bado mafanikio hayatatokea mara (more…)

UKURASA WA 06; Kazi Ndio Msingi Wa Maendeleo.

By | January 6, 2015

Tokea enzi na enzi za kuwepo kwa dunia haijawahi kutokea watu wakapata kila wanachotaka bila ya kufanya kazi. Hata wakati ambao watu waliishi kwa kula vyakula vya asili bado ilimbidi mtu kwenda kuwinda au kuzunguka msituni kutafuta mboga, matunda na vyakula vingine. Lakini kwa njia moja au nyingine dunia ya (more…)

UKURASA WA 05; Anzia Hapo Ulipo, Anza Na Ulichonacho.

By | January 5, 2015

Mabadiliko yoyote unayotaka kufanya kwa mwaka huu 2015 anzia hapo ulipo na anza na ulicho nacho. Usijidanganye unasubiri mambo yawe mazuri, ukweli ni kwamba hayatakuwa mazuri, kila siku ina changamoto zake. Kama umepanga kuanza biashara anza sasa, anza na kile ulicho nacho. Kama huna cha kuanza kabisa, fikiria kitu ambacho (more…)

UKURASA WA 04; Unacho Kila Unachohitaji Ili Kufanikiwa.

By | January 4, 2015

Kama ningekuwa na mtaji, basi ningeanzisha biashara kubwa sana na sasa hivi ungekuta nimeshafanikiwa. Kama ningekuwa najuana na watu waliofanikiwa wangenipa connection na mimi ningeshatoka Kama ningezaliwa kwenye familia yenye uwezo kama John ungekuta na mimi sasa hivi nina nyumba, gari na biashara kubwa. Kama bosi wangu asingekuwa na roho (more…)

Ukurasa Wa 03; KIFO…(Umuhimu Wake Na Jinsi Unavyoweza Kukitumia Kufikia Mafanikio)

By | January 3, 2015

Kuna siku utakufa, ndio unalijua hili ila kuna kitu kimoja hujajifunza kuhusiana na kifo chako. Leo kwenye ukurasa wa 03 wa kurasa 365 za mwaka 2015 utaandika kitu kimoja kikubwa unachoweza kujifunza kutokana na kifo. Baada ya muda utakufa na utakuwa umekufa kwa muda mrefu sana kuliko muda ulioishi. Kwa (more…)

UKURASA WA 02; Malengo.

By | January 2, 2015

Timu za Simba na Yanga zilicheza mpira kwenye uwanja wa taifa, katika mechi hii magoli yaliondolewa. Unafikiri ni nani aliibuka mshindi kwenye mchezo huu? Nahodha mmoja alipewa meli na aelekee popote meli itakapoenda. Hakupewa uelekeo wala ramani wala kituo anachotakiwa kufika. Aliambiwa akae tu kwenye meli na itakapomfikisha ndio hapo (more…)

KURASA YA 01; Maisha Unayoishi Ni Yako.

By | January 1, 2015

Katika ukurasa huu wa kwanza kabisa wa kitabu kipya ambacho ni mwaka 2015 ni muhimu sana kuyakubali maisha yako ili uweze kuyabadili. Kubali kwamba maisha unayoishi ni ya kwako na wewe ndio kiongozi mkuu wa maisha yako. Wewe ndio dereva wa gari unaloendesha ambalo ni maisha yako. Wewe kama dereva (more…)

Kurasa 365 Za Mwaka 2015, Fursa Muhimu Kwako Kujifunza.

By | January 1, 2015

Mwaka huu 2015 una siku 365, ya kwanza ndio tunaimaliza leo, hivyo zimebaki siku 364 tu. Chukulia siku hizi 365 kama kitabu kitupu chenye kurasa 365 na kila siku unapata nafasi ya kuandika kurasa moja kwenye kitabu hiki. Je utachagua kuandika nini kwenye kila kurasa? Je umeandika nini kwenye ukurasa (more…)