Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 158; Kabla Ya Kufanya Jambo Lolote Jua Kitu Hiki Muhimu.

By | June 7, 2015

Kuna mambo mengi sana unayohitaji kufanya na unayoweza kufanya kwenye maisha yako. Lakini sio mambo yote unayotaka kufanya ni muhimu kwako au yatakufikisha kwenye malengo uliyojiwekea. Hivyo ni muhimu sana kujua ni kitu gani unafanya na kina umuhimu gani. Hakuna kitu kinauma kama kufanya vizuri sana kitu ambacho hakikutakiwa kufanywa (more…)

UKURASA WA 157; Maisha Ya Kuzima Moto, Yajue Na Yaepuke

By | June 6, 2015

Watu wanaofanya kwenye idara ya zima moto kazi yao ni moja tu, kusubiri moto utokee na kwenda kuuzima. Kama hakuna moto, hawana kazi kubwa, ila moto unapotokea ndipo hufanya kila juhudi kuuzima. Sasa kuna watu wengi kati yetu ambao wanaishi maisha ya zima moto. Watu hawa wanaweza kuwa na malengo (more…)

UKURASA WA 156; Kabla Hujalalamikia Changamoto Unayopitia, Tafadhali Sana Soma Hapa.

By | June 5, 2015

Kuna wakati ambapo mambo yanaweza kuwa magumu sana kwako. Huu ni wakati ambapo unakuwa umeweka malengo na mipango yako ila unashindwa kuyafikia. Unapanga kufanya kitu fulani ili baadae upate majibu mazuri lakini hiyo pia haitokei. Wakati kama huu unaweza kujiona kama wewe una kisirani au huwezi kufikia kile unachotaka. Katika (more…)

UKURASA WA 155; Hii Ndio Sababu Kubwa Inayokufanya Ushindwe Kutatua Matatizo Yako.

By | June 4, 2015

Tumewahi kujadili hapa kwamba matatizo uliyonayo umeyatengeneza wewe mwenyewe. Hii inatokea kwa sababu kwa kila tatizo ulilonalo, unapojaribu kulitatua unatengeneza tatizo jingine. Kila suluhisho linakuja na tatizo jipya kabisa. Hivyo unaweza kuchagua ni matatizo ya aina gani unafanya. Kuna wakati mtu anaweza kuwa kwenye matatizo makubwa sana na akawa hajui (more…)

UKURASA WA 154; Jinsi Ya Kuwinda Fedha Zako Mwenyewe Ili Kufikia Uhuru Wa Kifedha.

By | June 3, 2015

Kwenye makala ya siku mbili zilizopita tuliona kwamba kila mtu anawinda fedha zako wewe. Kila mtu anayejaribu kukushawishi ununue kitu, kila anayekushawishi utoe fedha yako anaiwinda fedha yako. Kuna watu wengi sana wanaokuzunguka ambao wanawinda fedha yako, hivyo usipokuwa makini utashangaa umefanya kazi miaka mingi ila huoni kikubwa ulichobadili kwenye (more…)

UKURASA WA 153; Huyu Ndio Pekee Anayefanana Na Wewe Kwa Kila Kitu.

By | June 2, 2015

Katika dunia hii ambayo ina watu zaidi ya bilioni saba, kuna mtu mmoja tu ambaye anafanana na wewe kwa kila kitu. Hii ni kuanzia uwezo, ubunifu, vipaji na hata mipango mbalimbali ya kimaisha. Kwa kumjua mtu huyu na kushirikiana naye vizuri kutakuwezesha wewe kufikia mafanikio makubwa sana. Utafikia mafanikio makubwa (more…)

UKURASA WA 152; Kila Mtu Anawinda Kitu Hiki Muhimu Ulichonacho, Kuwa Makini.

By | June 1, 2015

Tunaishi dunia ambayo kila mtu kuna kitu anatafuta. Na kipimo kimoja ambacho kinapima kile ambacho kila mtu anataka ni fedha. Kama unataka kuwa na maisha yenye hadhi nzuri basi yatapimwa kwa kiwango cha fedha unachotengeneza au ulichonacho. Hivyo kwa kila wakati kila mmoja wetu anapambana kupata fedha. Tunafanya kazi na (more…)

UKURASA WA 151; Je Unazalisha Au Wewe Ni Mtumiaji Tu?

By | May 31, 2015

Katika dunia tunayoishi, kuna makundi mawili ya watu. Kuna kundi la watu ambao ni wazalishaji, hawa ni watu ambao wanatuletea vitu vyote tunavyotumia. Simu, tv, vyakula vizuri, vitabu, makala tunazosoma, nguo tunazovaa, magari na vingine vingi. Kundi la pili ni la watumiaji. Hawa ni watu ambao wanatumia vitu hivi vinavyotolewa (more…)

UKURASA WA 150; Sababu Moja Inayokufanya Unakwama.

By | May 30, 2015

Moja ya vitu vizuri nilivyojifunza kwenye maisha ni kwamba, watu huwa wanayafanya maisha yao kuwa magumu wao wenyewe. Yaani kama unaona maisha yako ni magumu, basi wewe mwenyewe umechangia sehemu kubwa sana ya ugumu huo. Unaweza kukataa na kusingizia kila kitu unachoweza, serikali ambayo haitoi ajira, uchumi ambao ni mgumu, (more…)

Ukurasa Wa 149; Hawa Ndio Watu Unaotakiwa Kuwafikiria Zaidi.

By | May 29, 2015

Utakapoamua kuboresha maisha yako, utakapoamua kufanya tofauti na ulivyokuwa unafanya na utakapoanza kupata majibu ya tofauti na uliyokuwa unapata mwanzo, kuna watu watakuchukia. Nataka nikuambie hilo wazi. Kuna watu watakuchukia wazi wazi na kukuambia huwezi au unapoteza muda wako, na hata ukiweza watakuambia subiri. Na kuna wengine watakuchukia kwa ndani (more…)