Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 148; Mambo Kumi(10) Unayotakiwa Kubadili Leo Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.

By | May 28, 2015

Kuna picha moja ya katuni ambapo kiongozi amesimama jukwaani na anawauliza wananchi, wangapi wanataka mabadiliko? Wote wananyoosha mikoni. Anauliza swali la pili wangapi wanataka kubadilika? Hakuna hata mmoja ananyoosha mkono. Hivi ndivyo maisha ya watu wengi yalivyo, kila mtu anataka mabadiliko, anataka maisha yake yawe bora, anataka kuwa na kazi (more…)

UKURASA WA 147; Njia Rahisi Ya Kufikia Uhuru Wa Kifedha.

By | May 27, 2015

Kama kichwa cha habari kimekuvutia na ukafikiri hapa utajifunza njia rahisi ya kupata fedha umekosea njia, hapa sikupi njia rahisi ya kupata fedha, haipo, kwa sababu kama ingekuwepo na jinsi ambavyo watu wanaipenda fedha kila mtu asingeijua. Hapa nataka nikushirikishe njia rahisi ya wewe kufikia uhuru wa kifedha. Unakuwa na (more…)

UKURASA WA 146; Ukiendelea Na Maisha Haya Watu Watakunyanyasa Sana…

By | May 26, 2015

Katika moja ya makala za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 tuliona kwmaba wewe mwenyewe ndio unaweza kutoa ruhusa ya mtu kukunyanyasa. Japokuwa ruhusa hii unaitoa pale unapokubali kunyanyasika na kitu anachofanya au anachosema mtu, kuna njia nyingine ya kunyanyasika ambayo hata kama hutakubali kuchukua kile ulichoambiwa au kufanyiwa bado utanyanyasika. (more…)

UKURASA WA 145; Kitu Pekee Unachoweza Kukidhibiti Kwenye Maisha Yako.

By | May 25, 2015

Mara nyingi huwa tunafikiri wkamba tunaweza kuwadhibiti watu, kudhibiti hali zinazotokea, kudhibiti fedha na mambo mengine mengi. Ila tunapojaribu kudhibiti vizu hivi tunashindwa vibaya sana. Kwa kushindwa huku tunaweza kujiona kama hatufai au hatuwezi kuendesha maisha yetu vizuri. Leo nataka nikuambie kwamba kushindwa kudhibiti vitu hivyo unavyotaka kudhibiti hakumaanishi kwamba (more…)

UKURASA WA 144; Huu Ndio Ukweli Kuhusu Wewe.

By | May 24, 2015

Leo nataka nikuambie ukweli kuhusu wewe, ndio wewe hapo una mambo mengi mazuri unayoweza ila unayakwepa. Kuna ukweli mwingi sana kuhusu wewe lakini umeamua kutokuufanyia kazi. Kwa kutojua ukweli huu na kutoufanyia kazi imekuwa kikwazo kwako kuboresha maisha yako. SOMA; Usijaribu Kumbadili Mtu, Utapoteza Muda Wako… Huu ndio ukweli kuhusu (more…)

UKURASA WA 143; Wewe Ni Sumaku…

By | May 23, 2015

Wewe ni sumaku inayoishi. Nafikiri unaijua sumaku, na unajua tabia za sumaku. Kama umesahau sumaku, ni chuma ambacho kina uwezo wa kuvuta vyuma vingine. Sumaku haiwezi kuvuta kila kitu, ila inaweza kuvuta vile vitu ambavyo vinatabia za kufanana na sumaku. Sumaku itavuta chuma, lakini haiwezi kuvuta plastiki. Wewe ni sumaku (more…)

UKURASA WA 142; Maisha Ni Mafupi, Usiyapoteze Kwa Kufanya Mambo Haya….

By | May 22, 2015

Miaka 100 ijayo kila mtu anayesoma hapa sasa hivi atakuwa amekufa. Kitachobaki kwenye dunia hii sio mipango mikubwa uliyokuwa nayo, na wala sio ahadi nyingi ulizoweka, bali ni jinsi gani uligusa maisha ya wengine kw akile ambacho ulikuwa unafanya. SOMA; Hiki Ndio Kitakachotokea Miaka 100 Ijayo.. Kama miaka 100 ijayo (more…)

UKURASA WA 141; Kama Huna Hofu, Una Tatizo Kubwa Sana.

By | May 21, 2015

Hofu imekuw akikwazo cha watu wengi sana kufikia mafanikio makubw akwneye maisha yao. Unajua kabisa hutaki kubaki hapo ulipo, unajua unataka uanze biashara, unajua unataka uanze kuweka ubora kwenye kile ambacho unafanya ili uweze kupata mafanikio makubwa. Unaweka malengo na mipango ya kukuwezesha kufika kule unakotaka kufika naunajua kila hatua (more…)

UKURASA WA 140; Usiwasamehe Wazazi Wako, Waelewe…

By | May 20, 2015

Kuna watu wengi sana ambao wanaamini maisha yao yalivurugwa na maamuzi ambayo wazazi wao waliyafanya siku za nyuma wakati wao bado ni wadogo. Watu hawa wamekua wakiishi na imani hii kwa muda mrefu na inazidi kuwazuia wao kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Kabla hata sijaweka maelezo mengi hapa, naomba (more…)

UKURASA WA 139; Huyu Ndio Mtu Pekee Anayeweza Kukunyanyasa.

By | May 19, 2015

Kuna wakati unaweza kuona kama watu wengine wanakunyanyasa au kukushambulia kutokana na hali uliyonayo au kitu unachofanya. Katika hali kama hii unachukua hatua gani? Unalalamika kwa nini watu wakushambulie wewe? Unajiona kama ni mtu mwenye bahati mbaya kutokana na hali ulizo nazo ambazo zinawafanya wengine wakunyanyase na kukushambulia? Kama hiki (more…)