Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 128; Ni Sawa Kama Hutapata Kile Unachotaka.

By | May 8, 2015

Kila mmoja wetu ana malengo na mipango yake kwenye maisha, na hiki ndio kitu ambacho kimekuwa kinakusukuma uweke juhudi zaidi kwenye kile unachofanya. Lakini hakuna ambaye ana uhakika wa kile ambacho kinaweza kutokea kesho. Na hii ndio sehemu muhimu ambayo unatakiwa kujipa ruhusa kwa sababu kushindwa kufanya hivyo utaishi maisha (more…)

UKURASA WA 127; Kinachokufanya Ukwame, Na Uwe Na Maisha Magumu.

By | May 7, 2015

Sehemu kubwa ya maisha yako kuwa magumu inasababishwa na wewe mwenyewe. Binadamu tumekuwa na tabia ya kufanya maisha yetu kuw amagumu kadiri siku zinavyozidi kwenda na kadiri tunavyofanikiwa. Chanzo kikuu cha maisha ya watu kuwa magumu ni kuishi maisha ya maigizo. Hakuna kitu kinachoweza kumuuziza mtu kama kuishi maisha ya (more…)

UKURASA WA 126; Mitandao Ya Kijamii, Kazi na Mapumziko.

By | May 6, 2015

Sasa hivi tunaishi kwenye dunia ambayo vitu vimekuwa havina ukomo tena. Sasa hivi unaweza kuwa na mawasiliano masaa 24 kwa siku na siku 7 kwa wiki. Mitandao ya kijamii inakuonesha kila kitu na kwa muda wowote. Imetokea ajali mbali huko, ndani ya dakika chache unazopicha zote za ajali. Ni maendeleo (more…)

UKURASA WA 125; Huoni Kwa Sababu Hutaki Kuona.

By | May 5, 2015

Kuna vitu vingi sana ambavyo vinatokea hapo ulipo. Kuna fursa nyingi sana ambazo zimekuzunguka. Kuna mambo mazuri sana kwenye maisha yako na hata kazi/biashara yako ambayo ukiweza kuyatumia vizuri yatakuletea mafanikio makubwa. SOMA; Kitu Pekee Kinachoweza Kuiharibu Siku Yako Na Jinsi Unavyoweza Kuepuka… Lakini wewe huyaoni. Huyaoni sio kwa sababu (more…)

UKURASA WA 124; Kuwa Tone La Asali…

By | May 4, 2015

Tone la asali linavutia inzi wengi kuliko ndoo nzima iliyojaa nyongo. Unapokuwa mwema na unapofanya mema unawavutia watu wengi kuliko unavyokuwa na ubaya na kutenda mabaya. Hata kama unafanya jambo dogo kiasi gani, kama ni jema endelea kulifanya litawafikia wengi na kuwasaidia wengi pia. Usifiche chochote kizuri ambacho unacho, usiogope (more…)

UKURASA WA 123; Kazi Kama Bidhaa…

By | May 3, 2015

Kazi au shughuli yoyote unayofanya ni sawa na bidhaa iliyopo sokoni, kama thamani yake kwa sasa haikuridhishi, ongeza uhitaji wake na thamani yake itakua. Watu wengi wamekuwa wakilalamika kwamba kazi wanayofanya inawapa kipato kidogo. Au biashara wanayofanya haiwapatii faida ya kutosha. Watu hawa huishia kulalamika tu bila ya kuchukua hatua (more…)

UKURASA WA 122; Dalili Kwamba Unaweza Kufikia Mafanikio Makubwa.

By | May 2, 2015

Moja ya vitu vinavyoweza kutuonesha kama kitu kinawezekana au hakiwezekani ni utafiti. Ndio maana kabla ya mtu kuingia kwenye biashara anahitaji kufanya utafiti ili kujua kama kuna wateja ambao wanahitaji huduma au bidhaa anazotoa. Hata kwenye sayansi, kabla kitu hakijapitishwa lazima ufanyike utafiti. Kabla dawa yoyote haijapitishwa kwa matumizi ya (more…)

UKURASA WA 121; Fanya Tukio Hili La Kihistoria Ambalo Litakupa Uhuru Uliopoteza.

By | May 1, 2015

Leo ni siku ya mwisho ya kujiunga na SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA. Kwa maelezo zaidi bonyeza HAPA. Kwa kiasi kikubwa sana umepoteza uhuru wako kwenye maisha. Kumbuka kipindi ulipokuwa mtoto ni mambo gani uliyokuwa unafikiria au kupanga? Ni ndoto zipi kubwa ulizokuwa nazo ambazo hukuona haya kuzisema mbele ya (more…)

UKURASA WA 120; Ni Muda Tu…

By | April 30, 2015

Nafikiri umewaona watu wengi ambao wamefanikiwa zaidi ya ulivyofanikiwa wewe. Na labda kuna wakati unajiona wewe umeshindwa kwa sababu tu hujafikia viwango vile ambavyo wengine wameweza kufikia. Au labda huna uwezo mkubwa, au labda huna bahati kama waliyonayo wengine. Yote haya sio ya kweli, hakuna mwenye bahati zaidi ya mwenzake (more…)

UKURASA WA 119; Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Hofu.

By | April 29, 2015

Hebu jiulize kama isingekuwa hofu leo hii ungekuwa wapi? Fikiria mipango yote ambayo umewahi kuwa nayo kwa muda mrefu lakini ilipofika utekelezaji tu, hofu ikabisha hodi na ikakufanya usidhubutu hata kuanza. Kumbuka jinsi ambavyo umekuwa unahofia kushindwa, umekuwa unahofia kukataliwa, umekuwa unahofia kwamba utapata hasara kubwa. Umeacha kufanya kile ulichopanga (more…)