Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 118; Kitu Pekee Kinachoweza Kuiharibu Siku Yako Na Jinsi Unavyoweza Kuepuka…

By | April 28, 2015

Kuna watu huwa wanasema kwamba siku zao zina kisirani, wengine husema wameamkia upande mbaya na maneno mengine mengi yanayoashiria kwamba kuna siku mbaya na siku nzuri. Tuchukue mfano, umeamka asubuhi na kwa bahati mbaya umeamka kwa kuchelewa, hivyo unaanza kujiandaa haraka haraka, unavaa nguo huku unafanya mambo mengine ili tu (more…)

UKURASA WA 117; Huyu Ndiye Mtu Ambaye Umasikini Huwezi Kumbugudhi.

By | April 27, 2015

Umasikini unapenda sana kuwabugudhi watu, lakini sio watu wote. Kuna watu ambao umasikini hupenda sana kuwasumbua. Watu hawa huteseka kwa kipindi kirefu wkenye maisha yao mpaka pale yanapokwisha. Watu hawa wanaishi maisha yao yote wakitamani kwmaba umasikini uondokane nao lakini jambo hilo linashindikana. Watu hao wanaamini kwamba wakipata fedha tu, (more…)

UKURASA WA116; Usiwasikilize Watu Hawa.

By | April 26, 2015

Kuna watu kazi yao ni kupinga tu. Yaani watu wa aina hii hakuna kitu unaweza kufanya waache kupinga au kukosoa. Na hata utaka[ojaribu kujitetea watayapinga maelezo yako pia. Ni muhimu sana kuwajua watu hawa na kutowapa nafasi kubw akwenye akili yako. Usiogope kuendelea na mipango yako kwa sababu tu mtu (more…)

UKURASA WA 115; Hivi Ndivyo Unavyojitengenezea Dharura.

By | April 25, 2015

Maisha sio dharura, ila sisi wenyewe huwa tunayafanya yawe dharura. Kama utakuwa na malengo na mipango yako, halafu ukaifanyia akzi kwa wakati, hakuna wakati wowote ambao utaona una dharura. Ila hutakuwa na mipango na kufanya mambo pale unapojisikia, kuna wakati utajikuta kwneye dharura kubwa sana. Na hapa ndipo matatizo yote (more…)

UKURASA WA 114; Tumia Vikwazo Ulivyonavyo Kufikia Mafanikio.

By | April 24, 2015

Watu wengi huamini kwamba ili uwezekufikia mafanikio basi unahitaji uwe na vitu vingi sana au uweze kufanya vitu vingi. Hii inaweza kuwa kweli ila kuna ukweli unaotakiwa kuujua na unaweza kukushangaza sana. Ukiwachukua watu wawili, na mmoja akawa ana vitu vingi na kuweza kufanya vitu mbalimbali, mwingine akawa na vitu (more…)

UKURASA WA 113; Fursa Zinaweza Kukupoteza…

By | April 23, 2015

Fursa Fursa Fursa….. Katika wakati wowote ule kwenye maisha yako na katika jambo lolote unalofanya, kuna fursa nyingi sana ambazo zimekuzunguka. Na kama ukiwa macho ndio fursa zinazidi kuwa nyingi. Kwa kuwa wewe ni mtu ambaye unataka kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa inabidi uzichangamkie fursa hizi, si ndio? (more…)

UKURASA WA 112; Njia Kuu Mbili Za Kuishi.

By | April 22, 2015

Kuna njia kuu mbili za kuishi maisha yako hapa duniani. Njia ya kwanza ni kuishi kama ambavyo watu wanataka wewe uishi. Ufanye yale ambayo watu wanakutegemea uyafanye hata kama sio yanayokufurahisha au sio muhimu kwako. Ufanye kile ambacho kila mtu anafanya hata kama huna msukumo wowote wa kufanya hivyo. Hii (more…)

UKURASA WA 111; Kama NINGE….

By | April 21, 2015

Kama NINGEanza biashara kipindi kile nilipokuwa na kazi na nguvu bado, leo maisha yangu yangekuwa bora sana…. Kama NINGEchagua kuishi maisha ninayotaka kuishi mimi na sio maisha ya kuiga, leo hii nisingejikuta kwenye matatizo makubwa…. Kama NINGEpata muda wa kutosha wa kukaa na wale ninaowapenda, maisha yangu yangekuwa na furaha (more…)

UKURASA WA 110; Ukomo Unaojiwekea Wewe Mwenyewe.

By | April 20, 2015

Mimi sio aina ya watu ambao wanaweza kufanikiwa kwenye biashara…. Mimi sio aina ya watu ambao wanapandishwa cheo kazini… Mimi sio aina ya watu ambao wanaweza kufikia mafanikio makubwa… Mimi sio aina ya watu ambao wanaweza kufanya mambo makubw akwneye maisha yao. SOMA; Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara (more…)

UKURASA WA 109; Ni Lipi Dhumuni Lako Kwenye Maisha? Langu Ni Hili Hapa.

By | April 19, 2015

Licha ya kuwa na malengo na mipango bado maisha yako yanahitaji kuwa na dhumuni. Dhumuni hili ni kile ambacho unataka maisha yako yawakilishe hapa duniani. Hivi ni vile ambavyo unataka maisha yako yawe kuhusiana na kile unachofanya. Dhumuni lako kwenye maisha ndio litakaloendelea kukumbukwa hata pale utakapokuwa umeondoka kwenye dunia (more…)