Tag Archives: MAFANIKIO KWENYE BIASHARA

BIASHARA LEO; Mtazamo Wa Kuvuna Na Mtazamo Wa Kujenga.

By | June 13, 2015

Katika biashara kuna mitazamo miwili mikubwa, mtazamo wa kwanza ni wa kuvuna, na mtazamo wa pili ni wa kujenga. Mtazamo wa kuvuna. Hapa ni pale ambapo mfanyabiashara anaangalia ni kitu gani anakipata sasa. Yeye anafikiria kuvuna tu na hivyo anapoipata fursa anaitumia kwa uhakika. Na kama hakuna njia ya kuvuna (more…)

BIASHARA LEO; Kutojali Kwako Kunavyokuletea Hasara Kwenye Biashara.

By | June 11, 2015

BIASHARA LEO; Kutojali Kwako Kunavyokuletea Hasara Kwenye Biashara. Jana nilikuwa kwenye ofisi moja, mama mmoja akatoka kwenda kutoa fedha kwa njia ya simu na kununua vocha pia. Baada ya muda alirudi akiwa amekamilisha zoezi lake na kutaka kuingiza vocha kwenye simu. Alipoangalia akakuta amepewa vocha mara mbili ya alizoagiza. Alinunua (more…)

BIASHARA LEO; Sehemu Mbili Anazokwenda Mteja Wako Unazotakiwa Kuzijua.

By | June 10, 2015

Unapokuwa kwenye biashara, jukumu lako kubwa ni kumjua mteja wako kuliko hata anavyojijua wewe mwenyewe. Labda sio, lakini cha msingi lazima umjue mteja wako vizuri. Changamoto nyingi za biashara zinaanza pale mfanyabiashara anaposhindwa kumjua mteja wake vizuri na hivyo anashindwa kwenda naye vizuri kwenye biashara yake. Kama unasema huna haja (more…)

BIASHARA LEO; Kama Sio Namba Moja Au Namba Mbili Acha Kupoteza Muda Wako.

By | June 5, 2015

Kwa haraka tu na bila ya kuzunguka zunguka nikuambie kwamba biashara unayofanya kama wewe sio namba moja, au sio namba mbili basi acha kupoteza muda wako kwenye hiyo biashara. Kama sio namba moja au namba mbili kwenye biashara unayofanya maana yake huna biashara yenye wateja wa kutosha, unapata wale wateja (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Inayolipa Kuliko Hiyo Unayofanya Sasa.

By | June 4, 2015

Katika wakati wowote kwenye maisha yako ya kibiashara, kuna biashara ambayo itakuwa inalipa kuliko biashara unayofanya wewe. Katika hali hii unaweza kushawishika kwamba biashara uliyopo wewe sio nzuri na kutamani kuwepo kwenye biashara ile ambayo inalipa. Na kuna baadhi ya watu huamua hata kufanya maamuzi ya kubadili biashara na kuhamia (more…)

BIASHARA LEO; Sababu Moja Kwa Nini Biashara Yako Haina Soko.

By | June 3, 2015

Kama biashara haina soko kuna jambo moja tuna uhakika nalo, itakufa. Hakuna biashara ambayo itaweza kujiendesha bila ya kuwa na wateja. Mafanikio yako wewe kama mfanyabiashara ni kiasi gani cha soko umeshika. Kuna biashara nyingi sana ambazo zinakufa kwa kukosa soko. Leo nataka nikupe sababu moja kwa nini biashara yako (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Hujaanza Biashara Yoyote Mpya, Zingatia Jambo Hili Moja Muhimu Sana.

By | June 2, 2015

Biashara mpya zina kasi kubwa sana ya kushindwa. Hapa kwetu Tanzania hatuna tafiti za kutosha ila kwa nchi zilizoendelea na zilizofanya tafiti, biashara 8 kati ya 10 zinazoanzishwa hufa mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Hii ni hatari sana na kwa uzoefu tu hapa kwetu hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Kuna (more…)

Tofauti ya biashara kubwa na biashara ndogo na jinsi ya kuitumia kukuza biashara yako.

By | June 1, 2015

  Wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wanafanya kosa moja kubwa sana linalogharimu ukuaji wa biashara zao. Kwa kufanya kosa hili wamekuwa wakishindwa kukuza biashara zao na hivyo biashara kufa au kubaki kwenye kiwango kilekile. Kosa kubwa ambalo wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wanafanya ni kufikiri kwamba biashara ndogo ni aina ndogo ya (more…)

BIASHARA LEO; Hiki Ndio Kikomo Cha Biashara Yako Kukua.

By | May 30, 2015

Biashara yako ina ukomo wake wa kukua, yaani biashara inaweza kukua mpaka itakapofikia ukomo huo utakaoujua leo. Bila ya kujua ukomo hii ni vigumu sana kwa biashara yako kuweza kukua zaidi. Wafanyabiashara wengi ambao biashara zao zimedumaa hawajui kwamba tayari zimefikia ukomo. Hivyo hukazana kufanya mambo mengi ambayo bado hayasaidii (more…)

BIASHARA LEO; Hapa Ndio Biashara Yako Inapokosa Maana…

By | May 25, 2015

Unapojaribu kuwa kila kitu kwa kila mtu biashara yako inakosa maana na unashindwa kuwa chochote kwa yeyote. Ufanye nini basi; kuna wa pekee kwa kundi fulani la watu. Usitake kumpata kila mteja aliyepo hapa duniani, bali lenga kuwapata wale watu ambao utaongeza maana kwenye maisha yao, utatatua matatizo yao na (more…)