Tag Archives: MAFANIKIO KWENYE BIASHARA

Jenga biashara yako kwenye misingi hii mitatu na itakuwa imara.

By | May 25, 2015

Kuna biashara nyingi ambazo zinaanzishwa lakini hazifiki mbali. Kuna biashara ambazo zimekuwepo kwa kitambo kirefu lakini hazina mabadiliko yoyote kwenye ukuaji, na baada ya muda zinakufa kabisa. Sio kwamba wanaoanzisha biashara hizi hawana mawazo mazuri, wengi wana mawazo mazuri ya biashara. Wengi wanakuwa wamefanya biashara yenye mafanikio lakini baada ya (more…)

BIASHARA LEO; Kama Bado Hujawa Tayari Kuingia Kwenye Biashara…

By | May 23, 2015

Watu wengi wamekuwa wakiniandikia kwamba wanataka kuanza biashara ila bado hawajawa tayari. Wanakuwa na sababu nyingi ambazo huzitumia na hufikiria wakimaliza mambo fulani kwanza ndio wataingia kwenye biashara. Sasa kama na wewe ni mmoja wa watu ambao wanafikiria kwamba bado hawajawa tayari kuingia kwenye biashara, nataka nikuambie kitu kimoja, hakuna (more…)

BIASHARA LEO; Tafuta Wenye Maumivu…

By | May 22, 2015

Unaweza kuw ana biashara nzuri sana, una bidhaa au huduma bora kabisa inayoweza kutatua matatizo ya mtu na kuboresha maisha yake. Ila kila unapomwambia mtu kuhusu biashara yako, au unapowatangazia watu ambao unaona wanafaa kuwa wateja wako, hawaonekani kuwa tayari kununua bidhaa au huduma hiyo. Katika hali kama hii ni (more…)

BIASHARA LEO; Kama Huwezi Kusema Kitu Hiki Kimoja, Huna Biashara.

By | May 20, 2015

Katika wakati wowote na popote ulipo ni lazima uweze kuielezea biashara unaofanya kwa sentensi moja. Ni lazima ndani ya dakika moja uweze kumweleza ni biashara ya aina gani unayofanya na inaelekea wapi, au ina mahitaji gani. Ukishindwa kufanya hivi basi hua biashara. Huna biashara kwa sababu huijui biashara yako vizuri (more…)

BIASHARA LEO; Kama Biashara Yako Isingekuwepo….

By | May 19, 2015

Leo kaa chini na ujiulize na kupata jibu la swali lifuatalo; Kama biashara yako isingekuwepo, je watu wanaokuzunguka wangekuwa katika hali gani? Je dunia ingekuwa kwenye hali gani? Kama jibu ni hakuna tofauti kati ya kuwepo au kutokuwepo kwa biashara yako, basi huna biashara, yaani upo tu unasukuma siku. SOMA; (more…)

Changamoto ya kuendesha biashara wakati bado umeajiriwa.

By | May 18, 2015

Ni hali iliyowazi kwamba maisha yanakuwa magumu kadiri siku zinavyokwenda. Na gharama za maisha zinaongezeka huku vipato vya Ajira vikibaki pale pale au kuongezeka kidogo sana. Hali hii imewafanya waajiriwa wengi kujiingiza kwenye ujasiriamali. Hivyo licha ya kipato cha ajira wanapata kipato kingine cha ziada kupitia ujasiriamali wanaofanya. Waajiriwa wanakuwa (more…)

BIASHARA LEO; Kinachokufanya Ushindwe Kutekeleza Mipango Yako.

By | May 16, 2015

Kila mfanyabiashara anayo malengo na mipango yake kwenye biashara anayofanya. Lakini ni wachache sana ambao wanaweza kufikia mipango yako na kuvuna matunda mazuri. Wafanyabiashara wengi huwa na mipango mizuri ila unapofika wakati wa utekelezaji ndio ugumu unaopoonekana. Hapa ndipo mtu anaona kama haiwezekani na kuamua kurudi nyume na kuendele akufanya (more…)

BIASHARA LEO; Usianze Biashara Upya Kila Siku…

By | May 13, 2015

Moja ya changamoto zinazowasumbua watu wengi kwenye biashara ni kuanza upya biashara kila siku na kila mara. Hali hii imefanya biashara zionekane ni ngumu sana kuliko ugumu wenyewe. Mtu anaanzaje biashara upya kila siku? Sio kwamba mtu anafunga biashara yake na kuanza upya, ila uendeshaji wake wa biashara unakua ni (more…)

Hii Ndio sababu halisi kwa nini biashara nyingi zinashindwa.

By | May 11, 2015

Huwa napata nafasi ya kukutana na kuwasiliana na wajasiriamali na wafanyabiashara mbalimbali. Na kikubwa nilichojifunza ni kwamba kwanza, watu wanakutafuta pale ambapo biashara imeshafikia hali ngumu sana kiasi kwamba inahitaji nguvu kubwa sana kuirudisha kwenye mstari. Na pili, watu wengi hawajui sababu hasa ya kushindwa kw abiashara zao, wanakuwa wana (more…)

BIASHARA LEO; Kuhusu Wateja Wasionunua Kwako.

By | May 8, 2015

Kwenye biashara unayofanya, kuna wateja ambao unajua kabisa wanaweza kunufaika na biashara yako, ila mpaka sasa hawanunui kwako. Je umewahi kujiuliza ni kwa nini? Kama bado unapoteza wateja wengi sana, hao unaowajua tayari na hata ambao bado hujawajua. Kwenye biashara, kama ilivyo kwenye maisha ya kawaida, hakuna kitu kinachotokea kw (more…)