Tag Archives: MAFANIKIO KWENYE BIASHARA

BIASHARA LEO; Tengeneza Mtandao Wako.

By | May 7, 2015

Kitakachokusaidia kufanikiwa kwenye jambo lolote sio kile ambacho unakijua bali wale ambao unawajua. Kadiri unavyojua watu wengi ndivyo unavyoongeza nafasi zako za kufanikiwa kwenye biashara yako. Ni muhimu sana kwako kukuza mtandao wako wa kibiashara. Hakikisha watu wengi unaowajua na hata usiowajua wanajua biashara yako. Hakikisha biashara yako unaweza kuieleza (more…)

BIASHARA LEO; Kama Mteja Anaweza Kununua Kwa Mtu Yeyote, Kwa Nini Anunue Kwako?

By | May 5, 2015

Swali rahisi sana; kama mteja anaweza kununua kwa mtu yeyote, kwa nini aje kununua kwako? Unaweza kujibu swali hili? Kama huwezi upo kwneye hatari. Ila usijali, nipo hapa ili tuweze kusaidiana ili uweze kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Kama mteja anaweza kununua kw amtu yeyote na hana sababu nyingine yoyote (more…)

BIASHARA LEO; Huwezi Kuwa Sahihi Mara Ya Kwanza.

By | May 4, 2015

Kuna swali ambalo huwa linaulizwa tena na tena na tena yaani kila siku swali hili linaulizwa. Hata nitakapomaliza kuandika hapa, mtu akipiga simu au kuandika email atauliza swali hilo. Swali lenyewe ni NIFANYE BIASHARA GANI AMBAYO INA FAIDA SANA, au NI BIASHARA GANI AMBAYO INALIPA SANA KWA SASA. Na jibu (more…)

Kabla hujahama biashara moja na kwenda nyingine zingatia mambo haya muhimu.

By | May 4, 2015

Moja ya mambo ambayo yanaulizwa sana na watu wengi wanaowasiliana na mimi kwa ajili ya ushauri ni kuhusu kuingia kwenye biashara nyingine. Yaani unakuta mtu anafanya biashara ya aina fulani na sasa anataka kuingia kwenye biashara ya aina nyingine. Watu wengi huanza kupata mawazo ya aina hii pale wanapoona biashara (more…)

Hii Ni Nafasi Ya Mwisho Kabisa, Usiikose Tena.

By | May 2, 2015

Kwanza niwashukuru sana wale wote ambao wameshajiunga na semina ya MAFANIKIO KATIKA BIASHARA  mwaka 2015. Umefanya maamuzi sahihi sana kujiunga na semina hii na utajifunza mambo mazuri ambayo kama utayatumia utaboresha zaidi biashara yako na kufikia mafanikio makubwa. Nimepokea ujumbe kutoka kwa watu wengi jana kusumbuliwa na mtandao hivyo kushindwa (more…)

BIASHARA LEO; Jambo Muhimu La Kila Mfanyabiashara Kufanya Kila Siku.

By | May 1, 2015

Leo ni siku ya mwisho ya kujiunga na SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA. Kwa maelezo zaidi bonyeza HAPA. Kujifunza kila siku ndio hitaji la chini kabisa ili kuweza kufikia mafanikio kwenye maisha. Na kwenye biashara hii ni muhimu zaidi kwa sababu mabadiliko makubwa yanatokea wkenye biashara kila siku. Kuna mbinu (more…)

BIASHARA LEO; PANGA MARA KUMI.

By | April 25, 2015

Uliisoma na kuielewa vizuri sheria ya mara mbili mara tatu? Kama hukuisoma ni muhimu sana wewe kufanya hivyo kwa sababu itakusaidia sana kwenye mipango yako ya muda na fedha kwenye biashara unayofanya. Unaweza kuisoma hapa; Tumia Sheria Ya Mara 2, Mara 3 Kwenye Mipango Yako Ya Biashara. Leo nakupa sheria (more…)

BIASHARA LEO; Pale Unaposikia “BIASHARA FULANI INALIPA SANA” Jua Umeshachelewa.

By | April 23, 2015

Kuna baadhi ya biashara huwa zinakwenda na misimu fulani. Kuna kipindi watu wanakuwa wanazungumzia sana biashara ya aina fulani, inapata umaarufu sana na kila mtu anakimbilia kuifanya. Hizi ni zile hadithi kwamba biashara fulani inalipa sana, ona watu fulani wamefanya na wamepata faida kubwa. Au kilimo fulani kinalipa sana, ona (more…)

Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.

By | April 20, 2015

Huu ni wakati ambao karibu kila mtu anahitaji kuingia kwenye biashara. Haijalishi mtu ameajiriwa au hana ajira, haijalishi kiwango cha elimu mtu alichonacho na wala haijalishi umri wa mtu, kwa sasa kila mtu anahitaji kuwa kwenye biashara. Ajira zimekuwa za shida kupatikana na hata wale wanaozipata bado haziwawezeshi kuyamudu maisha. (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Hajui Anachotaka, Ila Anajua Kitu Hiki Muhimu Sana.

By | April 16, 2015

Kama unataka kukuza biashara yako na ifikie viwango vya juu sana basi usitegemee sana maoni ya wateja, hasa kuhusu ni nini wanataka. Ukiondoa biashara za uchuuzi ambazo mtu anakwenda dukani moja kwa moja kununua sukari, biashara nyingi mteja hajui anachotaka. Ndio hajui ni kitu gani hasa anachokitaka, ila akikipata atafurahia (more…)