Tag Archives: MBINU ZA MAFANIKIO

Hivi ndivyo unavyoweza kuianza wiki yenye mafanikio.

By | November 17, 2014

Habari za asubuhi rafiki?Ni siku nyingine mpya na mwanzo wa wiki mpya.Naamini umeipangilia wiki yako vizuri kwa ajili ya kufikia mafanikio makubwa.Wiki hii fanya kitu hiki kimoja;Dhibiti kiwango cha taarifa unazopata, hasa kupitia vyombo vya habari. Hii ni kwa sababu taarifa nyingi ni;i. Zinakula muda wako mwingiii. Ni hasiiii. Hazina (more…)

Ushauri Muhimu Kwa Wanafunzi Wa Kidato Cha Nne.

By | October 31, 2014

Jumatatu ijayo tarehe 03/11/2014 wanafunzi wa kidato cha nne wanakwenda kuanza mitihani yao ya kuhitimu kidato cha nne. Hii ni hatua muhimu sana kwenye maisha yao kwani ndio itapelekea ndoto zao nyingine kuwa kweli. Kama mwananfunzi ana ndoto ya kuwa injinia, rubani, daktari au mwalimu, mitihani hii ni muhimu kwake (more…)

Kama Ulikuwa Hujui Bahati Inavyopatikana Soma Hapa.

By | October 23, 2014

Mara nyingi kwenye jamii zetu huwa tunawaona watu waliofanikiwa kama watu wenye bahati. Yaani walikutana na bahati ndio maana wamefikia mafanikio makubwa sana.Inaweza kuwa kweli ila hujui nini maana ya bahati.BAHATI NI PALE MAANDALIZI YANAPOKUTANA NA FURSA.Hivyo ili na wewe upate bahati una kazi mbili za kufanya;1. Kujiandaa kwa kiwango (more…)

Unataka Kufanya Biashara na Huna Mtaji? Unaweza Kuanzia Hapa

By | October 22, 2014

Moja ya vikwazo vinavyowazuia watu wengi kuanza biashara imekuwa ni mtaji.Japo mtaji sio kikwazo chenyewe, kuna mambo mengi yanawazuia watu kuingia kwenye biashara ila wao wanasingizia mtaji tu.Basi kama wewe unafikiri tayari una kila kinachohitajika ili iuweze kufanikiwa kwenye biashara kasoro mtaji tu, leo utajifunza baadhi ya biashara utakazoweza kuanza (more…)

TOFAUTI 17 Kati Ya Matajiri na Masikini(kwa nini masikini wanaendelea kuwa masikini na matajiri kuendelea kutajirika)

By | October 17, 2014

Unajua kwa nini masikini wanaendelea kuwa masikini na matajiri wanaendelea kutajirika? Hongera sana, leo utajua hapa; 1. Matajiri wanaamini wanatengeneza maisha yao, wakati masikini wanaamini maisha yanatokea. 2. Matajiri wanacheza mchezo wa fedha ili kushinda, masikini wanacheza mchezo huu ili kutopoteza,na mwishowe hawashindi. 3. Matajiri wamejitoa kweli na wana nia (more…)

Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.

By | October 16, 2014

Fedha ni muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Na kila mmoja wetu ana lengo la kuwa tajiri au ukipenda kuwa na uhuru wa kifedha. Na lengo hili ndio linatufanya tufanye kazi kwa bidii na maarifa. Japokuwa watu wengi wanafanya kazi kwa nguvu sana bado maisha yao ni magumu (more…)

Sheria 12 Kwa Wanaoanza Biashara Kutoka Kwa Bilionea Mark Cuban.

By | October 14, 2014

Mark Cuban ni bilionea wa kimarekani ambaye amepata sehemu kubwa ya utajiri wake kupitia mtandao wa intanet. Mark ameanzisha makampuni kadhaa ambayo ameyauza kwa makampuni makubwa ikiwepo kampuni yake ya Micro Solutions aliyoiuza kwa kampuni ya yahoo kwa dola bilion 5.1 mwaka 1999. Katika uzoefu wake wa biashara, anawashirikisha wanaopanga (more…)