Tag Archives: MBINU ZA MAISHA

USHAURI ADIMU; Usijenge Nyumba Kwenye Uwanja Wa Kukodi.

By | January 27, 2015

Usijenge nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi. Inaonekana rahisi sana kusema hivyo, na hivi kweli unaweza kufanya hivyo? Yaani mtu kakudoshishia uwanja wake, ufanyie shughuli zako kwa siku chache wewe ukaamua kujenga kabisa nyumba ya kudumu? Kwa akili ya kawaida huwezi kufanya hivyo, kwa sababu unajua unakaribisha matatizo. Mwenye uwanja (more…)

Yako Wapi Yale Maisha? Ni Wakati Wa Kulipa Deni Sasa.

By | January 26, 2015

Kila mtu alipokuwa mdogo alikuwa na picha kubwa sana ya maisha yake. Ulipokuwa mdogo mtu akikuuliza unataka kuwa nani ulikuwa unajibu bila ya wasi wasi wowote kile unachotaka kuwa. Ulikuw ana picha kubwa ya maisha yako, vile unataka yawe na kile unachotaka kutoa. Safari ikaendelea na mahala fulani mambo yakabadilika. (more…)

Kitu Muhimu Cha Kufanya Kabla Ya Kutumia Muda Au Fedha.

By | January 25, 2015

Muda una thamani kubwa sana kuliko fedha, hii ni kwa sababu ukipoteza fedha unaweza kupata nyingine ila ukipoteza muda huwezi kuupata tena. Ila muda na fedha vina tabia moja inayofanana, ukivitumia bila ya kuandika kwenye karatasi unavipoteza. Kitu muhimu cha kufanya kabla ya kutumia fedha au muda ni kupangilia matumizi (more…)

Jambo Moja La Kushangaza Kuhusu Maisha.

By | January 24, 2015

Jambo la kushangaza kuhusu maisha ni kwamba kila mtu anajua ni jinsi gani maisha ya mwenzake inabidi yawe ila hajui yakwake yanatakiwa kuwaje. Ndio maana ni rahisi sana mtu kutoa maoni kwa mtu kwamba anakosea au hajui anachofanya, wakati maisha ya huyo mtoa maoni pia yanahitaji marekebisho. Usianguke kwenye hili, (more…)

Jibu Swali Hili Na Fanyia Kazi Jibu Lako, Maisha Yako Yatabadilika Sana.

By | January 23, 2015

Hili ni swali la msingi sana ambalo kama ukiweza kujiuliza na ukajijibu kwa uaminifu basi maisha yako yatabadilika na kuwa bora sana. Msisitizo ni jibu kwa uaminifu na fanyia kazi majibu yako. Swali lenyewe ni hili; KAMA UNGEWEZA KUWA BORA SANA DUNIANI KWENYE KITU KIMOJA TU, UNGECHAGUA KITU GANI? Andika (more…)

Kama Sio Wewe Nani? Kama Sio Sasa Lini?

By | January 21, 2015

Kama sio wewe utakayebadili maisha yako unafikiri ni nani atakayefanya hivyo? Kama sio sasa utabadili maisha yako umafikiri ni lini utafanya hivyo? Usijidanganye kwamba kuna mtu atakayekuja kukutoa hapo ulipo, ni lazima nia hii itoke ndani yako. Usijidanganye kwamba utabadili maisha yako kesho, kesho haijawahi kufika. NI WEWE, NI SASA, (more…)

Kuna Makundi Matatu Ya Watu; Je Wewe Upo Kwenye Kundi Lipi Kati Ya Haya? Fungua Kujua.

By | January 20, 2015

Duniani kuna makundi matatu ya watu. Na watu wote duniani tunaingia kwenye moja wapo ya makundi haya. Kundi ulilopo linaweza kuw akiashiria kama utafikia mafanikio au la. Na habari njema ni kwamba unaweza kubadilisha na kwenda kwenye kundi jingine ambalo litakufikisha kwenye mafanikio unayotaka. SOMA; Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo (more…)

Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

By | January 19, 2015

Binadamu tunapenda kulalamika sana na hata kuwalaumu wengine. Hakuna mtu anayependa aonekane kwamba yeye ndio amechangia kusindwa kwa jambo fulani. Hivyo katika jambo lolote lile linalotokea watu hukimbilia kumtafuta mchawi, yaani mtu wa kulaumu. SOMA; Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku. Sasa kwa tabia hii ya kulalamika (more…)

Jambo Muhimu La Kufanya Leo Jumapili Usiku.

By | January 18, 2015

Jumapili ndio inaisha na kesho tunaanza wiki nyingine mpya. Kuna mambo mengi unaweza kufanya siku ya leo kabla haijaisha. Ila kuna jambo moja muhimu sana ambalo kama utashindwa kulifanya unaweza kupoteza wiki yako nzima. Jambo muhimu la wewe kufanya leo ni kuipangilia wiki yako. Jua ni mambo gani ambayo utahitaji (more…)

Acha Kuifanya Hali Mbaya Kuwa Mbaya Zaidi.

By | January 18, 2015

Mara kwa mara kwenye maisha tunakutana na matatizo. Baadhi ya matatizo haya yanaweza kuwa makubwa sana kiasi cha kutukatisha tamaa. Lakini mara nyingi matatizo haya huanza kidogo na sisi wenyewe kuyafanya kuwa makubwa zaidi. Moja ya njia tunayotumia kufanya hali mbaya kuwa mbaya zaidi ni kutumia hisia wakati unapokutana na (more…)