Tag Archives: MBINU ZA MAISHA

Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

By | January 14, 2015

Kuna kauli nyingi ambazo watu wengi hupenda kutumia. Katika kauli hizi kuna ambazo hutusukuma mbele na kutufanya tufikie malengo yetu. Pia kuna kauli nyingine zinaashiria kushindwa na kukata tamaa. Kauli hizi zinaweza kukuzuia kufikia mafanikio makubwa. Zifuatazo ni kauli mbili za kuacha kutumia leo ili kuweza kifikia malengo yako. 1. (more…)

Maisha Sio Rahisi Lakini Ni Mazuri Kama Hivi…

By | January 13, 2015

Maisha ni magumu, angalau hakuna anayeweza kulipinga hili. Maisha yatakuwa rahisi lini? Hayatakuwa rahisi, unafikiri ukipata kazi maisha yatakuwa rahisi, ndio zinaibuka changamoto nyingine nyingi. Unafikiri ukiongeza kipato maisha yatakuwa rahisi ila ukweli ni kwamba changamoto ndio zinazidi… Sasa kama maisha sio rahisi na hayatakuwa rahisi uzuri wake uko wapi? (more…)

Ulizaliwa na Uhuru Ila Hivi Ndivyo Ulivyoupoteza.

By | January 10, 2015

Msingi wa maisha ni uhuru wa kweli, ulizaliwa ukiwa na uhuru wa kila kitu kwenye maisha yako lakini jamii inayokuzunguka imekushawishi uuze uhuru wako ili kupata usalama. Kwa njia hii umepoteza uhuru wako wa kuamua kutengeneza maisha unayotaka mwenyewe. Na kibaya zaidi unakosa vyote, uhuru na usalama. Kujifunza zaidi jinsi (more…)

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumia Akili Yako Vizuri Na Ikakuletea Kila Unachotaka

By | January 9, 2015

Kama UTATUMIA AKILI YAKO VIZURI ni vigumu sana kushindwa kuishi maisha unayotaka. Tambua kikubwa ni kuweza KUTUMIA AKILI YAKO VIZURI. Na ni vigumu sana kuitumia akili yako hasa kwenye ulimwengu wa sasa ambao kila mtu anataka uangalie anafanya nini. Huyu anakutumia video ya vichekesho, yule anakutumia picha yaaani ni fujo (more…)

Ni Afadhali Kupotea Kuliko Kubaki Hapo Ulipo.

By | January 9, 2015

Moja ya vitu ambavyo vinawafanya wengi kuogopa kuchukua hatua ya kubadili maisha yao ni kuogopa kupotea. Yaani okuoghopa kushindwa au kuogopa hali kuwa mbaya kuliko ilivyo sasa hivi. Ukweli ni kwamba ni heri upotee kuliko ubaki hapo ulipo. Maana utakapopotea utajifunza na kujua ipi ni njia sahihi. Ukibaki hapo ulipo (more…)

Hakuna Anayejua Anachofanya, Na Huo Ndio Uzuri Wa Maisha.

By | January 8, 2015

Huenda kuna wakati ambao unafika na unahisi hujui ni kitu gani unafanya kwenye haya maisha. Na mara nyingi hutokea pale unapokumbana na changamoto au matatizo. Hali hiyo inaweza kukufanya hata ukate tamaa. Leo nina habari nzuri kwako, haupo mwenyewe, binadamu wote hakuna anayejua anachokifanya hapa duniani. Yaani hakuna mwenye uhakika (more…)

Binadamu Ni Viumbe Wa Kuhukumu, Hivi Ndivyo Unaweza Kuepuka Madhara Ya Hukumu Zao.

By | January 7, 2015

Hakuna ubishi kwamba binadamu ni viumbe wa kuhukumu. Kila mmoja wetu kwa wakati tofauti anahukumu wengine iwe ni kimya kimya au wazi wazi. Tonatofautiana tu viwango. Chochote utakachofanya watu watakuhukumu, Ukifanya vizuri watasema unajifanya mjuaji, ngoja uporomoke, na watadhubutu kukwambia muda sio mrefu utaanguka. Ukifanya vibaya watakusema wewe ni mzembe, (more…)

Kauli Mbiu Ya Mwaka Huu; JUST DO IT.

By | January 6, 2015

Yaani mwaka 2015 ukifika, nitabadilisha kabisa maisha yangu… Mwaka 2015 nitaanza biashara yangu… Mwaka 2015 nitaacha kunywa pombe… Mwaka 2015 nitaanza kufanya mazoezi…. Haya sasa mwaka 2015 ndio huu hapa na unaanza kuchakaa. Je umeshaanza kutekeleza yale uliyojiahidi? Kama bado unasubiri lini, kesho? Umechelewa. Au unasubiri mambo yawe mazuri, Hayatakuwa. (more…)

Sikukuu Zimesisha Sasa Kinachoanza Ni Kazi..

By | January 4, 2015

Wiki chache zilizopita zimekuwa wiki zenye sikukuu na mapumziko mengi. Tumekuwa na sikukuu za krismas na hata mwaka mpya. Katika sikukuu hizi watu wengi walipumzika na kupata starehe pia. Sasa msimu wa sikukuu unaisha rasmi leo na kesho jumatatu kazi zinaanza kwa kasi ya ajabu pia. Licha ya kuanza kwa (more…)

Kesho Jua Litachomoza Tena…

By | December 30, 2014

Kesho asubuhi jua litachomoza tena, kama lilivyochomiza leo, jana na siku zote zilizopita.  Hii ina maana kwamba haijalishi leo mambo yako yamekwenda vibaya kiasi gani, kesho ni siku mpya na unaweza kubadili maisha yako.  Kesho jua litachomoza tena hata kama kutakuwa ja mawingu.  Hii ina maana kwamba hata kama unapitia (more…)