Tag Archives: MBINU ZA MAISHA

Mambo Matano Ya Kushangaza Kuhusu Siku Ya Jumatatu

By | September 29, 2014

Jumatatu ni siku ya kwanza ya wiki. Ni siku ambayo watu wanatoka kwenye mapumzimko na kuanza tena wiki ya kazi. Na kwa kuwa watu wengi hawapendi kazi wanazofanya, jumatatu inaonekana kuwa siku mbaya sana. Haya ni mambo matano ya kushangaza ambayo hutokea sana siku za jumatatu tofauti na siku nyingine (more…)

Ushauri Kwa Wajasiriamali Kutoka Kwa Mwanzilishi Wa Facebook.

By | September 26, 2014

Mmoja wa waanzilishi wa Facebook Dustin Moskovitz, ambaye amekuwa bilionea kupitia kampuni hiyo, sasa anamiliki kampuni nyingine inayotoa ushauri kwa wajasiriamali na wanaotaka kuingia kwenye ujasiriamali. Anasema tofauti na vyombo vya habari vinavyoonesha kwamba ujasiriamali ni kitu cha ufahari na rahisi, ni kazi ngumu sana ambayo inahitaji ujitoe sana. Anasema (more…)

Mambo 10 Unayotakiwa Kujua Kuhusu Uwekezaji.

By | September 25, 2014

Moja ya njia za kuelekea kwenye utajiri ni kuwa mwekezaji. Unapokuwa mwajiriwa unawasaidia wengine kuwa matajiri. Unapojiajiri au kufanya biashara unaanza kujijengea utajiri. Unapokuwa mwekezaji unakuwa kwenye nafasi kubwa ya kufikia utajiri. Hivyo ni muhimu sana wewe kuwa mwekezaji. Ila kabla hujawa mwekezaji, JIONGEZE na mambo haya kumi muhimu unayotakiwa (more…)

Ukiacha Kuangalia Facebook Kila Mara Mambo Haya Matano Yatatokea.

By | September 24, 2014

Facebook ni mtandao mkubwa sana wa kijamii ambao unaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi. Facebook imekuwezesha kujuana na watu wengi, kukutana na marafiki mliopotezana zamani na hata kujifunza mambo mengi. Hata makala hi unaweza kuwa umeipata kupitia facebok. Pamoja na faida hizi, facebook imekuwa chanzo kikubwa cha watu wengi kupoteza (more…)

Sehemu Tano Unazoweza Kupata Mtaji Wa Kuanzia Biashara.

By | September 24, 2014

Kisingizio kikubwa cha watu kushindwa kuanza biashara kimekuwa ni mtaji. Kila siku watu wanalalamika wanapenda kuanza biashara ila mtaji hawana. Lakini wakati huo hawafanyi jitihada zozote za kupata mtaji huo au kuanza kidogo na kufikia makubwa. Kulalamika kwamba taasisi za fedha hazitoi mkopo kwa watu ambao hawana dhamana ni kupoteza (more…)

Mambo Matano(5) Ambayo Ni Marufuku Kufanya Kwenye Eneo La Kazi.

By | September 24, 2014

Kazi ndio msingi wa maendeleo. Na ili uweze kufikia mafanikio makubwa ni lazima ufanye kazi kwa bidii na maarifa. Sifa moja kubwa ya kufanikiwa kwenye kazi yoyote ni kupenda unachofanya. Kuna mambo mengi sana ambayo ukiyafanya kwenye kazi yako yanakuzuia kufikia mafanikio. Leo JIONGEZE mambo haya matano ambayo ni marufuku (more…)

Sababu 5 Kwa Nini Ni Marufuku Wewe Kukata Tamaa.

By | September 23, 2014

Katika maisha kuna wakati ambapo mambo huwa magumu sana. Ni katika nyakati hizi ambapo watu wengi hukata tamaa na kuacha kile ambacho walikuwa wanafanya. Kwa kukata tamaa unashindwa kufikia mafanikio na pia unaona maisha yako kama hayana maana. Leo JIONGEZE na sababu hizi tano kwa nini ni marufuku wewe kukata (more…)

Mambo 5 Muhimu Ya Kufanya Kabla Hujalala Leo.

By | September 22, 2014

Siku ya leo ndio inaelekea kuisha na kwa siku nzima ya leo umepitia mambo mengi sana. Kuna mengi umefanikiwa kufanya leo na pia kuna ambayo umepata changamoto kubwa. Hata kama siku yako ilikuwa mbaya kiasi gani, kuna mambo mazuri uliyojifunza kwa siku hii. Hapa kuna mambo matano muhimu unayotakiwa kufanya (more…)

Faida 5 za matikiti maji kiafya

By | September 22, 2014

Tikiti maji  ni tunda ambalo linapatikana kwa wingi sana katika maeneo mbalimbali. Hili ni moja ya tunda ambalo linapatikana kila msimu wa mwaka. Hata bei ya tikiti maji sio kubwa sana kiasi cha kwamba kila mtu anaweza kupata tunda hili. Kuna faida nyingi sana za kula tikitimaji. Hapa utazijua faida (more…)

Biashara 5 Unazoweza Kuanza Kufanya Bila Ya Kuwa Na Mtaji.

By | September 22, 2014

Kikwazo kikubwa cha watu wengi kuingia kwenye biashara kimekuwa ni mtaji. Japo sio kweli kwamba mtaji pekee ndio kikwazo, lakini wengi wanaamini mtaji tu ndio unawazuia. Lakini pia wakati huo ambao mtu hana mtaji hakuna juhudi kubwa anazofanya ili kuhakikisha anapata mtaji huo. Sasa kufupisha habari leo JIONGEZE na biashara (more…)