Tag Archives: MBINU ZA MAISHA

Mambo Matano(5) Ya Kufanya Siku Ya Jumatatu Ili Kuwa na Wiki Yenye Mafanikio.

By | September 22, 2014

Jumatatu ndio siku inayochukiwa na watu wengi kuliko siku nyingine yoyote ya wiki. Siku hii imepewa majina mabaya sana likiwemo BLUE MONDAY. Jumatatu ni siku ambayo watu wanatoka kwenye mapumziko na kuanza tena kazi. Ni siku ambayo watu wanajua kuna siku tano za kazi mbele, na kama hupendi kazi yako (more…)

Mambo Matano Ambayo Watu Waliofanikiwa Hufanya Mwisho Wa Wiki.

By | September 20, 2014

Kwa taratibu nyingi za kazi kwa walioajiriwa na hata aliojiajiri mwisho wa wiki huwa ni siku za mapumziko. Kwa walioajiriwa wanaweza kuwa na siku mbili za mapumziko na waliojiajiri wanaweza kuwa na muda mfupi zaidi ya hapo. Jinsi unavyoweza kutumia siku hizo za mwisho wa wiki inaweza kukufanya ufikie mafanikio (more…)

Hivi Ndivyo Mitandao Ya Kijamii Inavyoharibu Akili Yako, Kuwa Makini.

By | September 20, 2014

Tunaweza kukubali kwamba mitandao ya kijamii ndio mapinduzi ya sasa. Yaani kama ilivyokuwa mapinduzi ya viwanda, sasa tuna mapinduzi ya mitandao ya kijamii. Mitandao kama facebook, twitter, instagram, linked in na mingine mengi imekuwa sehemu ya maisha yetu. Mitandao hii imekuwa na faida kubwa sana, kuwaleta watu karibu zaidi ya (more…)

Faida Tano Za Muziki Kiafya Na Mziki Mzuri Unaoweza Kusikiliza Leo.

By | September 20, 2014

Watu wengi wanapenda kusikiliza mziki ili kuburudika, ila mziki una faida nyingi sana ukiacha kuburudika tu. Mziki una faida kiafya kwa yeyote anayesikiliza. Ila mziki tunaozungumzia hapa ni mziki laini. Zifuatazo ni faida tano za mziki kiafya. 1. Mziki husaidia hupunguza maumivu. Watu ambao wanateseka na maumivu makali wameonesha kupata (more…)

Faida Tano (5) Za Kulala(Kusinzia) Mchana.

By | September 19, 2014

Katika jamii zetu kulala mchana inaweza kuonekana kama uvivu. Yaani mtu anayelala mchana anaonekana ni mvivu na hapendi kazi. Kinyume na imani hii kulala mchana kuna faida kubwa sana kuliko ulivyowahi kufikiri. Leo utajifunza faida tano za kulala mchana na kama utaweza uweke ratiba hiyo kwenye kila siku yako. 1. (more…)

Mambo 10 Unayotakiwa Kuacha Kufanya Ili kuboresha Maisha Yako.

By | September 18, 2014

Maisha yetu ya kila siku yana changamoto nyingi sana. Lakini sehemu kubwa ya changamoto hizi tunasababisha wenyewe kutokana na maamuzi tunayofanya au tabia zetu wenyewe. Hapa kuna mambo kumi ambayo unatakiwa uache kuyafanya ili uweze kuwa na maisha bora. 1. Acha kulalamika sana kwenye maisha yako. Kulalamika hakutakusaida zaidi ya (more…)

Fanya Mambo Haya Matano Kila Siku Asubuhi Na Utakuwa Na Siku Yenye Mafanikio.

By | September 18, 2014

Kila siku inayoanza ni siku mpya kwako kuleta mabadiliko kwenye maisha yako na dunia kwa ujumla. Hijalishi siku ya jana ilikuwaje kwako, ila leo unayo kwenye mikono yako na ni uamuzi wako kama unataka kuifanya siku yenye mafanikio au unataka kuipoteza. Fanya mambo haya matano kila siku asubuhi na utakuwa (more…)

Mambo Matano(5) Ya Kufanya Wakati Unaelekea Kukata Tamaa.

By | September 17, 2014

Maisha yana changamoto nyingi sana. Kuna wakati mambo yanaweza kuwa magumu sana kwako na kuona kama vile huo ndio mwisho wa dunia. Huu ndio wakati ambao unakata tamaa na kuona haiwezekani tena. Kabla ya kufikia hali hii ya kukata tamaa kuna mambo matano ya kufanya ambayo yatabadili kabisa hali yako. (more…)

Faida 5 Za Kukimbia Dakika 5 Kila Siku.

By | September 17, 2014

Kila mtu anafahamu kwamba mazoezi ni kitu muhimu sana kwa afya njema na maisha kwa ujumla. Lakini inapokuja kwenye kufanya mazoezi, watu wengi hufikiri ni lazima kwenda kwenye eneo maalumu la mazoezi au kununua vifaa maalumu. Kwa hiyo ukosefu wa vifaa hivyo na ukosefu wa muda pia hufanya watu wengi (more…)

Mbinu 5 Zitakazokufanya Uwe Mbunifu Zaidi.

By | September 17, 2014

Iwe umeajiriwa au umejiajiri unalipwa kulingana na ubunifu wako. Kama unataka kulipwa zaidi, yaani kupata wateja wengi zaidi au kupata kipato kikubwa zaidi ni muhimu kila siku kuongeza ubunifu wako kwenye kile unachofanya. Hizi hapa ni mbinu tano zitakazokufanya uwe mbunifu zaidi; 1. Pata muda wa kupumzika. Tafiti zinaonesha kwamba (more…)