Tag Archives: NENO LA LEO

NENO LA LEO; Huu Ndio Mwanzo Wa Mwisho Wa Maisha Yetu.

By | January 8, 2015

Our lives begin to end the day we become silent about things that matter. –Martin Luther King Jr. Maisha yetu yanaanza kufikia mwisho pale tunapokaa kimya kwa mambo ambayo tunayajali. Kama kuna jambo ambalo unalijali sana kwenye maisha yako usilikalie kimya hata kama mambo ni magumu kiasi gani. Endelea kupigania (more…)

#NENO_LEO; Huwezi Kumaliza Ubunifu Wako Kwa Kuutumia.

By | January 7, 2015

You can’t use up creativity. The more you use, the more you have. –Maya Angelou Huwezi kumaliza ubunifu wako kwa kuutumia. Jinsi unavyozidi kuutumia ndivyo unavyozidi kuongezeka. Tumia sana ubunifu wako kuboresha maisha yako, utumie pia kuwasaidia wengine. Habari mbaya kwako ni kwamba usipoutumia kabisa unaweza ukaupoteza. Nakutakia siku njema. (more…)

NENO LA LEO; Kitu Hiki Kimoja Kitakufanya Uache Kukosoa Wengine

By | January 6, 2015

Let the refining and improving of your own life keep you so busy that you have little time to criticize others. –H. Jackson Brown, Jr. Fanya jukumu la kubadili na kuboresha maisha yako liwe muhimu sana kwako na lichukue muda wako mwingi kiasi kwamba ukose muda wa kukosoa wengine. Binadamu (more…)

NENO LA LEO; Haijalishi Ni Mwendo Gani Unao Bali…

By | January 5, 2015

It does not matter how slowly you go as long as you do not stop. –Confucius Haijalishi una mwendo mdogo kiasi gani iwapo hutosimama. Kukimbia kwa kasi sana halafu ukasimama ni mbaya kuliko kwenda taratibu na bila ya kusimama. Unapoanza jambo lolote ni muhimu kukomaa nalo mpaka ufikie mafanikio. Hata (more…)

NENO LA LEO; Hawa Ndio Watu Wenye Furaha Zaidi.

By | January 4, 2015

Remember that the happiest people are not those getting more, but those giving more. –H. Jackson Brown, Jr. Kumbuka kwamba watu wenye furaha zaidi sio wale wanaopokea vingi bali wale wanaotoa vingi. Huwezi kuwa na furaha kwa kuwa mtu wa kupokea tu. Ukishakuwa mtu wa kupokea tu unaweza kujiona wa (more…)

NENO LA LEO; Gharama Ya Elimu Na Gharama Ya Ujinga.

By | January 3, 2015

Education costs money. But then so does ignorance. –Sir Claus Moser Elimu inagharimu fedha, vile vile hata ujinga unagharimu fedha. Gharama ya elimu utailipa kwa muda mfupi. Gharama ya ujinga utailipa miaka yako yote. Hakikisha kila siku unajifunza, hili ndio hitaji la chini sana la kuweza kufikia mafanikio. Nakutakia siku (more…)

NENO LA LEO; Umuhimu Wa Kuchepuka…

By | January 2, 2015

Without deviation from the norm, progress is not possible. –Frank Zappa Bila ya kuchepuka ni vigumu kuona mabadiliko/mafanikio. Kama unafanya kile ambacho kila mtu anafanya, utaishia kupata matokeo ambayo kila mtu anapata. Na mara nyingi matokeo ambayo kila mtu anapata ni ya kawaida. Hivyo unapokwenda na kundi unaishia kuwa wa (more…)

NENO LA LEO; Wazazi Wanavyojenga Au Kubomoa Maisha Ya Watoto Wao

By | December 31, 2014

It is not what you do for your children, but what you have taught them to do for themselves, that will make them successful human beings. –Ann Landers Sio kile unachowafanyia wanao ndio muhimu, bali kile ulichowafundisha kufanya kwa ajili ya maisha yao ndio kitawafanya wafanikiwe. Umekuwa ni utamaduni wa (more…)

NENO LA LEO; Njia Isiyokuwa Na Foleni.

By | December 30, 2014

There are no traffic jams along the extra mile. –Roger Staubach Hakuna foleni unapokwenda mbali zaidi. Unapofanya kile ambacho kila mtu anafanya utakutana na ushindani mkubwa sana. Unapofanya kitu chenye ubora mkubwa na wa kipekee utakuwa mwenyewe na hakutakuwa na ushindani. Mara zote nenda maili ya ziada, fanya zaidi ya (more…)

NENO LA LEO; Hiki Ndio Unachohitaji Ili Kufanikiwa.

By | December 29, 2014

In order to succeed, your desire for success should be greater than your fear of failure. –Bill Cosby Ili kufanikiwa, hamu yako ya mafanikio inabidi iwe kubwa kuliko hofu yako ya kushindwa. Kinachokufanya mpaka sasa hujafanikiwa ni hofu ya kushindwa. Una hofu kwamba ukijaribu kitu fulani unachokifikiria utashindwa. Ili ufanikiwe (more…)