Tag Archives: NENO LA LEO

NENO LA LEO; Ili kushinda Unahitaji Hiki, Na Kama Huna Utakipata Hivi.

By | March 7, 2015

To be a great champion you must believe you are the best. If you’re not, pretend you are. -Muhammad Ali Kuwa mshindi ni lazima uamini kwamba wewe ni bora. Na kama sio bora basi jifanye kuwa bora. Ushindi unaanzia ndani yako, kwa kuamini kwmaba wewe ni bora na unaweza kufanya (more…)

NENO LA LEO; Kitu Muhimu Kuvaa Kuliko Nguo.

By | March 6, 2015

Nothing you wear is more important than your smile. – Connie Stevens Hakuna kitu muhimu unachoweza kuvaa kama tabasamu. Muda wote vaa tabasamu, hapana sio muda wote, ila tabasamu ni muhimu. Tabasamu linakarisha watu, tabasamu linaleta ushirikiano na tabasamu linaonesha kujali. Zawadi bora unayoweza kumpa mtu ni tabasamu. Na silaha (more…)

NENO LA LEO; Hakuna Uhaba Wa Fursa.

By | March 5, 2015

There is far more opportunity than there is ability. -Thomas A. Edison Kuna fursa nyingi sana kuliko uwezo wa watu kuzitumia fursa hizo. Usidanganyike kwamba hakuna fursa, fursa zipo nyingi sana. Kama mpaka sasa hivi huzioni fursa maana yake uwezo wako bado uko chini kuliko fursa zinazokuzunguka. Kama utaongeza uwezo (more…)

NENO LA LEO; Ushauri Bora Unaoweza Kutoa Kwa Rafiki Yako.

By | March 4, 2015

“In giving advice, seek to help, not please, your friend.” – Solon Katika kutoa ushauri, toa ushauri utakaosaidia na sio ushauri utakaomridhisha rafiki yako. Hii ni changamoto kubwa sana hasa pale rafiki yako anapokosea. Mara nyingi utaogopa kumwambia kwa sababu unafikiria anakuchukuliaje. Au rafiki anakuomba ushauri na kwa maelezo yake (more…)

NENO LA LEO; Elekeza Uso Wako Hapa.

By | March 3, 2015

“Keep your face always toward the sunshine – and shadows will fall behind you.” —Walt Whitman Mara zote elekeza uso wako kwenye mwanga wa jua na kivuli kutaanguka nyuma yako. Angalia lile lililojema kwenye maisha yako na mabaya yataanguka nyuma. Usipoteze muda wako kuangalia mabaya, hakuna utakachofaidika nacho. Nakutakia siku (more…)

NENO LA LEO; Faida Ya Kuwasha Taa Yako…

By | March 2, 2015

As we let our own light shine, we unconsciously give other people permission to do the same. -Marianne Williamson Jinsi unavyoacha mwanga wako ung’ae ndivyo unawapa ruhusa watu wengine nao kung’arisha mwanga wao. SOMA; Matatizo Yote Kwenye Maisha Yako Yanatokana Na Kitu Hiki. Unapokazana na kupata mafanikio, ndivyo unavyowapa wengine (more…)

NENO LA LEO; Angalia Hapa…

By | March 1, 2015

It is better to look ahead & prepare than to look back & regret. -Jackie Joyner-Kersee Ni bora kuangalia mbele na kujiandaa kuliko kuangalia nyuma na kujutia. Jana imeshapita, jambo lolote ulilofanya jana huwezi kulibadili tena, ila unaweza tu kujifunza. Kesho bado haijafika, ila unaweza kuishi vizuri leo na kujiandaa (more…)

NENO LA LEO; Akili Ndogo, Akili za Kawaida Na Akili Kubwa.

By | February 28, 2015

Great minds discuss ideas; average minds discuss events; small minds discuss people. -Eleanor Roosevelt Akili kubwa zinajadili mawazo; akili za kawaida zinajadili matukio; akili ndogo zinajadili watu. SOMA; UKURASA WA 40; Amua Kuwa Wewe… Je wewe unajadili nini? Ukijikuta unajadili watu, fulani kafanya hiki, fulani kafanya kile na mengine mengi (more…)

NENO LA LEO; Vitu VIWILI Ambavyo Tayari Unavyo Na Vinavyoweza Kukufikisha Popote Unapotaka KWENDA.

By | February 27, 2015

You have brains in your head, and feet in your shoes. You can steer yourself any direction you choose.” Dr. Seuss Una ubongo kwenye kichwa chako na una miguu kwenye viatu vyako. Unaweza kuenda uelekeo wowote unaochagua. Tumia akili yako vizuri, kuwaza na kujua ni kitu gani hasa unachotaka kwenye (more…)

NENO LA LEO; Tatizo La Kuwa Na Machaguo Machache.

By | February 26, 2015

To the man who only has a hammer, everything he encounters begins to look like a nail. -Abraham Maslow Kwa mtu ambaye ana nyundo tu, kila kitu anachokutana nacho kinaonekana kama msumari. Kama unajua kitu kimoja tu, kila tatizo utakalokutana nalo utajaribu kulitatua kw akile unachojua. Na mara nyingi utatuzi (more…)