Tag Archives: SIRI 50 ZA MAFANIKIO

SIRI YA 30 YA MAFANIKIO; Uaminifu Unalipa Gawio Kubwa.

By | February 24, 2015

Watu wasioona mbali hawaelewi kwamba kila wanachofanya kina matokeo yake. Matendo mazuri yanapewa zawadi na matendo mabaya yanaadhibiwa. Ni bora kushindwa na ukabaki na heshima kuliko ukafanikiwa huku ukiwa tapeli.    “To measure a man, measure his heart.”  – Malcolm Forbes (more…)

SIRI YA 29 YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kupata Furaha.

By | February 23, 2015

Huwezi kutafuta furaha. Furaha ni zao la mambo haya matatu; 1. Ubora wa mahusiano yako na wengine. 2. Kiwango cha udhibiti ulionao kwa hisia zako. 3. Jinsi unavyotumia zawadi na uwezo wako katika kutimiza malengo yako. Kama unataka kuwa na furaha fanya kazi ya kuboresha mahusiano yako, dhibiti hisia zako (more…)

SIRI YA 28 YA MAFANIKIO; Tabia Zako Zitakujenga Au Kukubomoa.

By | February 21, 2015

Tabia zako zitakupeleka kwenye mafanikio au kushindwa. Ndio maana kuchangamana na washindi na kusoma vitabu vizuri ni muhimu sana. Kwa sababu unakuwa na tabia za watu unaokaa nao muda mrefu. Unaiga tabia zao. Na tabia ndio zinaamua mafanikio yako.   “The books you read and the people you meet will (more…)

SIRI YA 27 YA MAFANIKIO; Amua Kujiendeleza Kila Siku.

By | February 21, 2015

Watu waliofanikiwa sana kwenye kila eneo ni watu wanaojifunza kila siku na kila mara. Mara zote wanasoma vitabu, kusikiliza vitabu vya kuwaelimisha na kuhudhuria semina. Wanajua kwamba kama wakijifunza na kutumia yale waliyojifunza wanazidi oiuwa bora zaidi ya wale wanaoshindana nao. Kama utatumia dakika 15 mpaka 30 kwa siku kujisomea, (more…)

SIRI YA 26 YA MAFANIKIO; Mara Zote Weka Malengo.

By | February 21, 2015

Dhumuni la malengo ni kutupa umakini na mwelekeo. Akili yako haiwezi kukutafutia majibu kama haijawekwa kwenye uelekeo husika. Pale unapokuwa na malengo thabiti miujiza inatokea. Unaanza kupokea mawazo na fikra zinazokufikisha kwenye lengo lako. Maisha bila malengo yanakera. Maisha yenye malengo ni kama safari nzuri. Andika malengo yako kila siku (more…)

SIRI YA 25 YA MAFANIKIO; Ni Lazima Upande Kabla Hujavuna.

By | February 20, 2015

Ni lazima upande mbegu kabla ya kuvuna mazao. Unavyopanda mbegu nyingi zaidi ndivyo unavyovuna mazao mengi zaidi. Ukipanda mbegu kiganja kimoja, utavuna gunia moja, ukipanda bakuli moja utavuna magunia kumi. Mara zote unavuna zaidi ya unachopanda. Usihukumu kila siku kwa mavuno unayopata, bali hukumu kwa mbegu unazopanda. Je wewe unapanda (more…)

SIRI YA 24 YA MAFANIKIO; Fanya Licha Ya Kuwa Na Hofu.

By | February 20, 2015

Kama utasita kwa sababu ya hofu, hofu itaendelea kukua. Kama utafanya kile unachohofia hofu itapotea yenyewe. Kwa sababu hofu ni hali ya akili. Ni kama moshi tu. Usikubali hofu ikutawale. Itokomeze hofu kwa vitendo. Ujasiri ni kuweza kufanya licha ya kuwa na hofu. Woga ni kukimbia hofu zako. Je wewe (more…)

SIRI YA 23 YA MAFANIKIO; Kama Una Matumaini Ya Baadae Una Nguvu Leo.

By | February 19, 2015

Matumaini yanaona visivyoonekana na kufanikisha visivyowezekana. Napoleon alisema kwamba kazi ya kwanza ya kiongozi ni kuwapa watu wake matumaini. Kwa sababu watu wanapokuwa na matumaini, watapigania ndoto zao. Na wanapokosa matumaini wanakata tamaa. Zungukwa na watu ambao wanakutia moyo, watu watakaopanda matumaini na imani ndani yako na utaweza kuwa chochote (more…)

SIRI YA 22 YA MAFANIKIO; Ongeza Kazi Yako Ya kushindwa na Utaongeza Mafanikio Yako.

By | February 19, 2015

Watu waliofanikiwa wanakubali kushindwa kama sehemu ya maisha na wamaamua kutymia kushindwa kwao ili kufanikiwa. Wanaangalia kila kikwazo kama somo la kujifunza ili kufanikiwa. Wanaelewa kwamba kushindwa ni sehemu ndogo katika mchakato wa kufikia mafanikio na hawakubali iwe kikwazo kwao kufikia mafanikio.   “Failure is only the opportunity to more intelligently (more…)

SIRI YA 21 YA MAFANIKIO; Tegemea Kilicho Bora.

By | February 18, 2015

Pale unapoamini jambo linawezekana na kulifanyia kazi ipasavyo, dunia yote itakusaidia kufanya ndoto zako, malengo yako na mipango yako kuwa kwenye uhalisia. Wale wanaoshinda ni wale wanaofikiri wanaweza. Amini unaweza, tegemea makubwa, yafanyie kazi na utayapata.   “If you paint in your mind a picture of bright and happy expectations, (more…)