Tag Archives: SIRI 50 ZA MAFANIKIO

SIRI YA 10 YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujiamini.

By | February 6, 2015

Kujiamini kunatokana na maandalizi mazuri. Kujiamini hakutokani na “kujifanya mpaka utakapokuwa” Kujiamini kunatokana na kufanya kitu mpaka unakuwa mtaalamu, unabonea. Pale unapobobea kitu, unajiamini. Na unapojiamini unaweza kuanza kukamilisha vitu ambavyo hujawahi kufikiri ungeweza kukamilisha.   “Confidence does not come out of nowhere. It’s the result of something…hours and days (more…)

SIRI YA 9 YA MAFANIKIO; Lenga Jitihada Zako Zote Sehemu Moja.

By | February 6, 2015

Amua ni kitu gani muhimu kwako na lenga nguvu zako zote katika kukipata. Unapolenga nguvu zako zote kwenye lengo moja, nafasi ya kupata mafanikio ni ya uhakika mkubwa. Ukilenga nguvu zako kwenye malengo mawilu, nafasi yako ya kufanikiwa inashuka na kufikia asilimia 66. Ukigawa nguvu zako kwenye malengo matatu nafasi (more…)

SIRI YA 8 YA MAFANIKIO; Amini Kila Kinachotokea Ni Kwa Sababu Muhimu.

By | February 6, 2015

Jifunze kuangalia jambo jema kwenye kila tatizo unalokutana nalo. Kuna mambo mazuri sana unayoweza kujifunza kwenye kila changamoto. Changamoto zipo ili kutupunguza mwendo na tuweze kujifunza mambo muhimu ya kutusaidia kufikia ndoto zetu. “I always turn every disaster into an opportunity.”  – John Rockefeller (more…)

SIRA YA 7 YA MAFANIKIO; Fikiria Mawazo Ya Kukujenga.

By | February 5, 2015

Kile unachofikiri kinaamua ni nini utafanya. Kila unachofikiri kila mara kitaamua ni wapi utakapoishia na maisha yako. Hii ndio sababu kubwa kwa nini ni muhimu wewe kushirikiana na watu wenye mawazo ya mafanikio. Kwa kutengeneza timu ambayo mtashirikiana na kusaidiana, utajitengenezea uhakika wa kufanikiwa. “What’s going on in the inside (more…)

SIRI YA 6 YA MAFANIKIO; Tumia Nguvu Yako Kuchagua.

By | February 5, 2015

Haijalishi upo katika hali gani, unayo nguvu ya kuchagua ni jinsi gani hali hiyo itakuathiri. Una nguvu ya kuchagua watu unaotaka kushirikiana nao. Una nguvu yankuchagua jinsi utakavyotumia muda wako. Una nguvu ya kuchagua ni vitabu gani usome. Una nguvu ya kuchagua ni hatua gani utachukua dakika tano zijazo ili kujisogeza (more…)

SIRI YA 5 YA MAFANIKIO; Jiamini Na Utaweza Kufikia Ndoto Zako.

By | February 3, 2015

Kama unwamini kitu kinawezekana na mtizamo wako ni kuwa tayari kufanya chochote na kwa muda wowote kukipata, basi mafanikio kwako ni swala la muda tu. Kwa hali hii unakuwa na uhakika wa kufikia mafaniko kwenye jambo lolote unalofanya. Unaweza kujiongezea kujiamini kwa kusoma vitabu vya kujijenga, kusoma blogs za kukufundisha (more…)

SIRI YA 4 YA MAFANIKIO; Itumie Sheria Ya Wastani Kukuletea Mafanikio.

By | February 2, 2015

Jinsi unavyoshindwa mara nyingi ndivyo unavyojitengenezea nafasi kubwa ya kufanikiwa. Kwa kifupi unaweza kutumia kushindwa kwako, kufikia mafanikio. Kila mara unaposhindwa unapata uzoefu, na unajifunza njia gani haileti matokeo mazuri. Pia unaepuka kurudia makosa ambayo yamekufanya ushindwe. “I am not discouraged, because ever wrong attempt discarded is another step forward.” (more…)

SIRI YA 3 YA MAFANIKIO; Mtazamo Wako Utaamua Mafanikio Yako.

By | February 2, 2015

Mtazamo wako ni picha ya akili yajo. Ni jinsi ambavyo unaona vitu. Mafanikio yako yatatokana na kile unachoona, iwe unaona uwezekano au unaona changamoto. Kuwa na mtizamo chanya hakukuhakikishii mafanikio. Lakini unaookuwa na mtizamo chanya una nafasi kubwa ya kufanikiwa. “Things turn out the best for the people  who make (more…)

SIRI YA 2 YA MAFANIKIO; Tumia Chochote Kitakachokuwezesha Kufikia Malengo Yako.

By | February 1, 2015

Watu wenye mafanikio mara zote wanatafuta chochote kitakachowawezesha kufikia malengo yao. Watu wenye mafanikio wanaangalia mbele ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuzitumia fursa zinazojitokeza mbele yao. Anza kuangalia mbele. Fikiria mbele na panga mbele, utakuwa katika nafasi nzuri ya kutumia fursa zitakazojitokeza wakati wengine wakiwa bado wanasinzia. “The (more…)

SIRI YA 1 YA MAFANIKIO; AMUA KUFANIKIWA.

By | February 1, 2015

Siri ya kwanza kabisa ya wewe kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni kuamua kufanikiwa. Amua kwamba maisha yako yatakuwa bora zaidi ya yalivyo sasa. Pia kuwa tayari kulipa gharama ya mafanikio. Watu waliofanikiwa wanajua ili kufanikiwa kuna gharama unatakiwa kulipa. Weka malengo, fanya kazi kwa juhudi na maarifa, kuwa (more…)