Tag Archives: USHAURI ADIMU

Faida kumi za kuwa na MAONO kama nilivyojifunza kwenye kitabu THE PRINCIPLES AND POWER OF VISION.

By | April 7, 2015

Rafiki yangu Meshack Maganga​​ alinipa zawadi ya kitabu hiki. Aliniambia ni kitabu kizuri sana. Nikawa na shauku kubwa ya kukisoma na hatimaye nimekisoma na kwa kweli ni kitabu ambacho sijui kwa nini nimechelewa kukisoma. Ni kitabu chenye misingi yote ya kukuwezesha kufikia kile unachotaka kwenye maisha. Na hata kama hukijui (more…)

Njia Moja Ya Uhakika Ya Kuishinda Hofu.

By | March 28, 2015

Ili kuishinda hofu, rudisha mawazo yako kwenye wakati uliopo sasa. Maana hofu kubwa unaipata pale unapofikiri mambo yaliyopita ambayo huwezi kuyabadili na kuwaza mambo yajayo ambayo huwezi kuyabadili pia. Acha kuwaza mambo ambayo yameshapita, huwezi kuyabadili. Yatakuumiza na kukupa hofu kubwa. Acha kufikiria mambo yajayo na kuyahofia. Bado hujayafikia na (more…)

USHAURI ADIMU; Tangaza Kazi Yako, Usione Aibu Wala Kujali Wengine Watakuonaje.

By | March 14, 2015

Katika moja ya changamoto kubwa sana ambayo watu wanaipata na inawazuia kufikia mafanikio ni kushindwa kutangaza kazi zao. Na hii inakwenda sana kwa wale ambao wanafanya kazi binafsi. Kwa mfano kama unapika mandazi matamu sana, ila anayejua kuhusu mandazi hayo ni wewe na familia yako tu, je nafikiri unabiashara hapo? (more…)

Hii Ndio Hatari Kubwa Ya Zama Hizi Tunazoishi..

By | March 11, 2015

Kama ulisoma historia wakati upo shuleni utakuwa unakumbuka kwamba binadamu amepitia vipindi vingi sana mpaka kufikia hapa tulipo sasa. Kwanza kabisa binadamu alianza kwa kula mizizi na majani, baadae akawa anawinda, baadae akaanza kulima ikaendelea hivyo mpaka sasa maisha yanaonekana kuwa bora zaidi. Binadamu tumepitia zama nyingi sana. Tumepita zama (more…)

Kama Una Vipaumbele Huna Kipaumbele…

By | March 1, 2015

Kama una vipaumbele maana yake ni huna kipaumbele. Kama una vitu vingi ambavyo ni muhimu kwako maana yake huna ambacho ni muhimu kwako. Kipaumbele maana yake ni kitu kimoja unachokipa upendeleo na kukifanya kabla ya kufanya kitu kingine. Sasa kama una kipaumbele zaidi ya kimoja, maana yake hakuna ambacho ni (more…)

USHAURI ADIMU; Kwa Sababu Umelipia Haimaanishi Utumie Yote.

By | February 25, 2015

Siku hizi ukinunua kifurushi cha mawasiliano kwenye mitandao ya simu, unapewa meseji 250 kwa siku. Ukisema utume meseji zote hizi, hata kama utatumia dakika moja kutuma meseji itakuchukua dakika 250 ambazo ni sawa na masaa manne. Sasa kama utatumia masaa manne kutuma meseji kwa siku kila siku inabidi uwe unafaidika (more…)

USHAURI ADIMU; Chukua Ushauri Kwa Mtu Huyu Tu, Achana Na Wengine Wote.

By | February 24, 2015

MSOMAJI; Nimekuwa nikisoma baadhi ya makala zako. Naomba nikuulize. Je, mtu unapoamua kufanya biashara fulani,ukaomba ushauri kwa watu,hao watu kwa uoga wao wakakuvunja moyo kuwa utakuwa kwenye risk zaidi. Unaionaje hii?asante,naamini utanijibu niweze kuelewa. MIMI; Usiombe ushauri kwa mtu ambaye hafanyi biashara, atakudanganya. Usiombe ushauri kwa mtu aliyepata hasara kwenye (more…)

Sababu Namba Moja Kwa Nini Hufanikiwi Kwenye Kazi Unayofanya.

By | February 21, 2015

Sababu namba moja kwa nini hufanikiwi kwenye kazi unayofanya ni kwa sababu unaangalia fedha tu. Yaani wewe kinachokusukuma ufanye kazi ni kwa sababu unapata fedha. Sasa fedha inapokuwa ndio hamasa kwako utafanya kile tu ambacho kinakuletea fedhq, hutataka kwenda hatua ya ziada na hivyo kujinyima fedha nyinhi zaidi baadae. Ufanyeje (more…)

Faida Kumi Za Kujisomea Ukiacha Kuongeza Maarifa.

By | February 19, 2015

Naweza kusema sasa hivi nimekuwa mlevi wa kitu kimoja, kusoma. Na sio kusoma tu, bali kusoma vitu vizuri ambavyo vinanifanya kuwa tofauti, kufikiri tofauti na hata kupata maarifa zaidi. Naweza kusema kw akujivunia kwamba chochote ninachofanya sasa kinatokana na maarifa makubwa ninayoyapata kwa kusoma vitabu. Nasoma vitabu vingi na kwa (more…)

Mambo Yamebadilika, Hatari Sio Hatari Tena, Salama Ndio Hatari…

By | February 11, 2015

Kuna wakati ambapo ilikuwa inaonekana kuacha kazi na kuingia kwenye ujasiriamali ni hatari kubwa sana. Ajira zilikuwa na usalama, angalau mtu alikuwa na uhakika wa kupata kipato cha kumtosha kuendesha maisha yake. Ila sasa hivi mambo yamebadilika kabisa, hatari sio hatari tena, na salama imekuwa hatari, tena hatari kweli kweli. (more…)