Tag Archives: USHAURI ADIMU

USHAURI ADIMU; Usijenge Nyumba Kwenye Uwanja Wa Kukodi.

By | January 27, 2015

Usijenge nyumba yako kwenye uwanja wa kukodi. Inaonekana rahisi sana kusema hivyo, na hivi kweli unaweza kufanya hivyo? Yaani mtu kakudoshishia uwanja wake, ufanyie shughuli zako kwa siku chache wewe ukaamua kujenga kabisa nyumba ya kudumu? Kwa akili ya kawaida huwezi kufanya hivyo, kwa sababu unajua unakaribisha matatizo. Mwenye uwanja (more…)

USHAURI ADIMU; Unapokutana Na Tatizo Jiulize Jambo Hili Moja La Msingi.

By | January 21, 2015

Tukubaliane kwamba lazima utakutana na matatizo. Katika jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako, iwe ni kazi au biashara kuna wakati utakutana na matatizo. Iwe matatizo hayo umesababisha wewe au hujasababisha una swali hili muhimu la kujiuliza? Je kuna suluhisho la tatizo hili? Kama suluhisho lipo huna haja ya kuhofu anza (more…)

Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

By | January 19, 2015

Binadamu tunapenda kulalamika sana na hata kuwalaumu wengine. Hakuna mtu anayependa aonekane kwamba yeye ndio amechangia kusindwa kwa jambo fulani. Hivyo katika jambo lolote lile linalotokea watu hukimbilia kumtafuta mchawi, yaani mtu wa kulaumu. SOMA; Haya Ni Maajabu Ya Dunia Ambayo Unayafanya Kila Siku. Sasa kwa tabia hii ya kulalamika (more…)

Acha Kuifanya Hali Mbaya Kuwa Mbaya Zaidi.

By | January 18, 2015

Mara kwa mara kwenye maisha tunakutana na matatizo. Baadhi ya matatizo haya yanaweza kuwa makubwa sana kiasi cha kutukatisha tamaa. Lakini mara nyingi matatizo haya huanza kidogo na sisi wenyewe kuyafanya kuwa makubwa zaidi. Moja ya njia tunayotumia kufanya hali mbaya kuwa mbaya zaidi ni kutumia hisia wakati unapokutana na (more…)

USHAURI ADIMU; Najua Kitu Kimoja….

By | January 18, 2015

Najua kitu kimoja… kwamba sijui chochote. Kauli hii tatanishi ilitolewa na mwanafalsafa Socrates. Kauli hii inaushauri muhimu sana kwetu; 1. Kama kuna kitu kimoja muhimu ambacho unatakiwa kujua ni kwamba hujui chochote. 2. Jiulize kwa kile ambacho unafikiri unakijua, na utagundua kwamba hukijui maka ulivyofikiri unakijua. 3. Huwezi kujua kila (more…)

Habari Za Kusikitisha; Kila Kitu Kinabadilika…

By | January 16, 2015

Leo nilipanda dala dala ambapo nilikaa kiti cha nyuma ya dereva, dereva alikuwa na mazungumzo na mtu mmoja aliyekaa mbele, anaonekana ni kondakta au dereva ila sio wa gari hiyo niliyopanda. Hivyo kwa sehemu yote ya safari walikuwa wakihadithiana ni jinsi gani anzi hizo kazi ya daladala inalipa. Waliongea sana (more…)

Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.

By | January 16, 2015

Kama utaamua kupuuza ushauri mwingine wowote ambao unausoma sehemu mbalimbali basi shika ushauri huu mmoja tu. Shikilia ushauri huu na kila siku jikumbushe maana ni muhimu sana kwako ili kuweza kufikia ndoto zako. Hii ni kwa sababu tunaishi kwenye jamii ambayo inajaribu sana kuturudisha nyuma. Huenda mwaka huu 2015 umeweka (more…)

Una Mdomo Mmoja Na Masikio Mawili Kwa Sababu Hii Kubwa.

By | January 13, 2015

Kila mtu ana mdomo mmoja na masikio mawili kwa sababu kuu moja; unatakiwa kusikiliza zaidi ya unavyoongea. Kwa bahati mbaya sana watu tunapenda sana kuongea badala ya kusikiliza. Unapokuwa muongeaji sana, unakosa kujifunza kutoka kwa wengine. Unapokuwa msikilizaji unajifunza mengi sana kutoka kwa wengine. Na kama una upumbavu mwingi ndani (more…)