Tag Archives: USHAURI WA BIASHARA

Tatizo la kuajiri wafanyakazi wasio na sifa kwenye biashara yako.

By | July 13, 2015

Mapinduzi ya viwanda yaliyotokea takribani karne mbili zilizopita yalileta mabadiliko makubwa sana kwenye ufanyaji wa kazi. Kabla ya hapo hakukuwa na ajira rasmi na hivyo watu wengi walizalisha kwa kiwango kidogo na kubadilishana. Viwanda vilipokuja viliweza kuzalisha kwa kiwango kikubwa sana na hivyo kuhitaji wafanyakazi wengi. Na kwa kuwa wafanyakazi (more…)

BIASHARA LEO; Je Biashara Yako Inaendana Na Wateja Wako?

By | July 10, 2015

Tulishasema kwamba jambo muhimu kabisa kwenye biashara ni kujua mteja wako ni nani. Kama upo kwenye biashara na humjui mteja wako basi hujui ni nini unafanya kwenye biashara yako. Na ninaposema kumjua simaanishi kumjua kwa jina, bali kujua sifa za mteja wako kuanzia umri, kipato, anakoishi na mengine kama hayo. (more…)

BIASHARA LEO; Hili ndio tatizo la kushindana kwa bei na linavyokumaliza.

By | July 9, 2015

Tatizo la kushindana kwa bei kwenye biashara ni kwamba linawamaliza wote mnaoshindana. Watu wengi huwa wanafikiri kwamba kwa kuweka bei ndogo basi ndio wanavutia wateja wengi. Hivyo wanaweka bei ndogo na mwanzoni wateja wanakuja kweli, baadae mshindani wako naye anashusha bei na wateja wanaenda kwake tena. Mnafanya mchezo huu kwa (more…)

BIASHARA LEO; Je Umemridhisha Mteja Wako Leo?

By | July 8, 2015

Kama jibu lako ni sina mteja basi jitathmini vizuri. Kwanza kabisa kila mmoja wetu ana mteja, kama wewe ni mtu mzima na unaishi basi una mteja au una wateja wengi sana. Wateja hawaishii kwa wafanyabiashara tu. Wateja wapo kwa kila mtu. Kama wewe ni mfanyabiashara, mteja wako au wateja wako (more…)

SABASABA, mambo muhimu kwa kila mfanyabiashara kutafakari kwenye msimu huu.

By | July 6, 2015

Tarehe saba ya mwezi wa saba kila mwaka ni sikukuu ya wafanyabiashara. Ni siku maalumu ambayo imetengwa na serikali kwa ajili ya wafanyabiashara kuazimisha kile ambacho wamekuwa wanafanya kwenye biashara zao. Msimu huu wa sabasaba kila mwaka hutawaliwa na maonesho ya kibiashara kwenye viwanja mbalimbali nchini. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitumia (more…)

BIASHARA LEO; Sikiliza Hawa Watu Wanaokupa Mawazo Ya Biashara Kila Siku.

By | July 3, 2015

Nikimaliza kuandika hapa na mtu akasoma, bado ataniandikia kwamba anatafuta wazo la biashara. Yaani wazo la biashara limechukuliwa kama ni kitu kikubwa sana ambacho watu wanapigana nacho ili wakipate. Ni kama ukishapata wazo basi mambo yako yote yamenyooka. Nimekuwa nikisema mara kwa mara mwamba wazo la biashara linaanza na wewe (more…)

BIASHARA LEO; Hiki Ndio Kitu Pekee Kitakachoifanya Biashara Yako Ndogo Iweze Kumudu Ushindani.

By | July 1, 2015

Kama unaendesha biashara ndogo, au unaendesha biashara mpya ambayo tayari kuna watu wengine ambao wanaifanya biashara hii kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko wewe, basi una njia nyembembe sana ya kuweza kufanikiwa. Ukweli ni kwamba hawa waliopo kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko (more…)

BIASHARA LEO; Mpango Wa Biashara Sio Biashara.

By | June 30, 2015

Nina mpango mzuri sana wa biashara, biashara hii itakuwa na wateja wengi na itatengeneza faida kubwa. Asante kwa mpango huo mzuri, lakini elewa kwamba mpango wa biashara sio biashara. Unaweza kuandika vizuri sana kwenye karatasi zako mteja wako ni nani, yupo wapi na utawezaje kumfikia, lakini hii sio biashara. Sisemi (more…)

Umuhimu wa mafunzo kwa wafanyakazi wa biashara yako.

By | June 29, 2015

Kama unafanya biashara kubwa maana yake una watu wengi ambao wanakusaidia kwenye biashara hiyo. Biashara yako haiwezi kukua na kuendelea kama huna watu wazuri ambao wanafanya kazi kwenye biashara hiyo. Na hata kama una biashara ndogo malengo yako ni kukua zaidi ya hapo ulipo sasa. Ili kukua utahitaji kuwa na (more…)

BIASHARA LEO; Mpe Mteja Chaguo Mbadala.

By | June 27, 2015

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakipoteza wateja kwa kushindwa kufanya kitu rahisi sana, kutoa chaguo mbadala kwa wateja wako. Kwa mfano mteja amekuja anataka kitu fulani ambacho wewe huna, badala ya kumwambia tu mimi sina hicho na aondoke, unaweza kumwambia sina hicho unachotaka ila kuna hiki kingine ambacho kinafanya kazi sawa na (more…)